Saturday, December 26, 2020

Joett Vocal Drills Vol. 1-7 sasa zinapatikana Internet Archive


Mazoezi yangu ya Joett Vocal Drills Vol. 1-7 sasa yanapatikana Internet Archive. Unaweza ku-download na vile vile ku-stream. Kama kuna maswali yoyote, naomba unijulishe.

Maelekezo ya haya mazoezi bado utayakuta kwenye makala yangu, Msaada wa Mafunzo ya Sauti na JOETT WhatsApp na Telegram, ila kwenye swala zima la ku-download, kwavile Mkito inasumbua sana (nadhani Mkito inaenda kufa) wewe nenda ka-download Internet Archive bila gharama yoyote. Ni bure. Nimeweka na links za Internet Archive uko kwenye hiyo makala yangu ya awali pia.

ANGALIZO - tafadhali tumia makala yangu ya awali kupata maelekezo ya kina pamoja na link ya video yangu yenye mifano ya Vol. 1-4. 

MP3 nilizopandisha Internet Archive ni tofauti na zile ya Mkito kwa maana hazina maelekezo ya ziada kwa lugha ya Kiswahili, yana mifano ya kila zoezi tu. 

Kwahivyo, maelekezo utayakuta kwenye makala yangu, Msaada wa Mafunzo ya Sauti na JOETT WhatsApp na Telegram.

Ku-download MP3 kwenye simu weka kidole kwenye track, kuna kadirisha katapanda, halafu chagua Download linkUkishindwa ku-download MP3 kwenye simu, tumia computer ku-download zip file. Ni option ya chini kabisa VBR MP3..

Internet Archive Download Link (hapo chini)
Nawatakia mafanikio mema,


JOETT - Mwalimu wa Sauti


JOETT - Got U On My Mind (Acoustic)

No comments:

Post a Comment