Saturday, November 10, 2018

Msaada Maalum wa Mafunzo ya Sauti na JOETT Kupitia Telegram


Kwa kipindi kirefu nimejaribu kusaidia watu kwa maelekezo, lakini mara kwa mara maswali yanakua yanajirudia. Kwanza kabisa, ni muhimu kuwaelewesha ya kwamba mazoezi ya sauti yana ratiba na miongozo ni lazima ifuatwe ndio upate mafanikio.

Swala hili nime elezea kwa kina hapa! (Kuna link za kubofya ambazo zitakupeleka kwenye maelekezo ya kina).

Leo ningependa kuorodhesha tu, yale ambayo utayakuta Joett Vocal Drills Vol. 1-4 kwenye mazoezi yangu yapatikanayo Mkito.com. Lakini pamoja na hilo, ningependa pia kuwakaribisha kwenye Channel yangu ya Telegram ambapo utakuta link ya kujiunga na Group langu la Telegram. Madhumuni ya hili group ni kutoa msaada kwa wale ambao wana nia na shauka la kujifunza kuimba vizuri. Unaweza kuuliza maswali na pia nitatupia maelekezo na mifano hapo. Ni juu yako wewe kutumia hii fursa au laa. Huduma hii natoa bure kabisa. Haina gharama yeyote. Ahsanteni.

1. Download Telegram App
2. Regista
3. Jiunge na Channel kupitia https://t.me/JoettMusic ambapo utakuta link ya kujiunga na Group la Joett Voice Studio.


Jifunze Kuimba na Joett Mkito.com: Vocal Drills Volume 1

Kwa awamu nyingine tena, na tena safari hii kwa maboresho yalio fuata mahitaji muhimu katika kujifunza kuimba kupitia mtandao, ninawaletea toleo mpya kabisa Jifunze Kuimba na Joett Mkito Volume 1. Hili toleo ni muhimu katika kukuwezesha kuingia katika mstari wa mafunzo ambayo bila shaka, yatakuletea mafanikio ya haraka. Kabla ya kuanza, hakikisha una download na kufanya zoezi langu la pumzi Mkito. Bila ya kuzungumza maneno mengi, nataka niwaachie toleo hili la kwanza (Vol. 1) msikilize mifano nakuendelea na mchanganyiko wa mazoezi ya sauti kwa takriban dakika 8. Mifano ipo. Nikusikiliza tu na kufuata hiyo mifano, na la msingi kabisa nikuachia sauti ifuate mkondo wake. Usilazimishe sauti. Iachie ifuate kinanda na maelekezo mwanana. Ukiwa na maswali, jiskie huru kuniuliza kwenye group langu la Telegram, au soma nakala kadhaa nilizo andika kwenye blog langu hapa! 

Jifunze Kuimba na Joett Mkito.com: Vocal Drills Volume 2

Volume 2 ni muendelezo wa Vol. 1. Kwa maana ni lazima ufanye Vol.1 kabla haujafanya Vol. 2. Kwa mara nyingine tena, nita sistiza mfuate maelekezo kama yalivo kwenye toleo hili. Mazoezi haya yana dakika 7. Ukishaweza kufanya haya mazoezi, sasa utakua na mazoezi mawili. Yaani Vol. 1 & 2 katika ratiba yako ya mazoezi ya sauti ya kila siku; na utatakiwa kufanya yote kwa pamoja kufuata mlolongo huo huo wa Vol. 1 kuingia Vol. 2. Kumbuka, madhumuni ya haya mazoezi ni ku re-balance sauti yako, au kurekebisha matumizi ya sauti yako ili uweze kuimba kwa urahisi kwenda juu na kwenda chini; na mpangilio na ratiba hii ndio itaweza kukupa wewe huo uwezo kwa njia ya haraka na salama zaidi. Tafadhali usianze kukurupuka na ku-download vitu olela kwenye internet. Tafadhali fuata maelekezo yangu na mazoezi niliokuandalia ili uweze kupata mafanikio ya uhakika.

Jifunze Kuimba na Joett Mkito.com: Vocal Drills Volume 3

Mazoezi ya Vocal Drills Volume 3 ni muendelezo wa Vol. 2. Kwa mara nyingine tena, fuata maelekezo. Kama unayo maswali ama kuna kitu kinakushinda, tafadhali uliza. Nitaweza kukupa ushauri. Lakini cha msingi nikufuata maelekezo na kufanya mazoezi stahiki kama nilivowaandalia hapa. Ukishaweza haya mazoezi ambayo muda wake ni takriban dakika 5, unatakiwa kuunganisha Vol. 1, 2 & 3 katika ratiba yako ya mazoezi ya sauti ya kila siku.

Jifunze Kuimba na Joett Mkito.com: Vocal Drills Volume 4

Volume 4 ndio toleo la mwisho katika awamu hii mpya ya Jifunze Kuimba na Joett Mkito. Fuata maelekezo. Panapokupa taabu, tafadhali niulize nikupe muongozo. Ukishaweza hili zoezi la takriban dakika 10, sasa utakua unamazoezi ya sauti Vol. 1, 2, 3 & 4 katika ratiba yako ya kujifunza kuimba. Kwahivyo, kilamara unapo kaa kufanya mazoezi yote haya kwa pamoja, unapaswa kufanya zoezi la pumzi kabla ya Vol. 1 alafu kuendelea na mazoezi ya Vol. 2, 3 & 4 bila ya kusimama.

Jumla ya muda wa mazoezi ukiunganisha hizi Volume zote 4 ni dakika 30. Kumbuka, madhumuni ya haya mazoezi ni ku re-balance sauti yako, au kurekebisha matumizi ya sauti yako ili uweze kuimba kwa urahisi kwenda juu na kwenda chini; na mpangilio na ratiba hii ndio itaweza kukupa wewe huo uwezo kwa njia ya haraka na salama zaidi. Tafadhali usianze kukurupuka na ku-download vitu olela kwenye internet. Tafadhali fuata maelekezo yangu na mazoezi niliokuandalia ili uweze kupata mafanikio ya uhakika.

Jifunze Kuimba na Joett Mkito.com: Vocal Drills Volume 5-7 

Vol. 5, 6 & 7 ni mazoezi ambayo yatakupeleka kutumia sauti kwenye nyimbo yangu Color Me Beautiful (Acoustic Pop) kwa mpangilio ulioupata wa matumizi stahiki ya sauti kutoka Vol. 1 - 4. Ni muhimu sana USIGUSE haya mazoezi mpaka baada ya muda...hata ikibidi miezi au wiki kadhaa, punde sauti yako imekaa sawa.

Nilicho kifanya hapa nikujaribu kuwezesha watanzania wote popote walipo, kupata mafunzo stahiki ya sauti bila ya gharama ya kuhudhuria mafunzo ya sauti darasani pamoja na mimi. Maelekezo na mazoezi haya ni nyeti kwa kukuwezesha kufikia malengo yako. Sikiliza. Tenda. Utapata faida kubwa sana kwenye swala la kuimba. Amini hilo!

Muongozo wa Mazoezi

  • Download mazoezi https://mkito.com/artist/1402419
  • Weka kwenye CD/Computer/Smartphone 
  • Tumia chombo cha muziki cha kupigia CD; au kama unatumia smartphone, computer au flash disk hakikisha unatumia external speakers
  • Fanya mazoezi ndani ya chumba na sio maeneo ya wazi, wala sio kwa kutumia speaker za simu yako ya mkononi wala headset za masikio.

Nawatakia mafanikio mema!


JOETT
Mwalimu wa Sauti

No comments:

Post a Comment