Tuesday, December 22, 2020

Yajue Makundi Haya Mawili ya Wasanii Waimbaji


Kuna waimbaji au wasanii wa kuimba wa aina mbili… kwa mtazamo wangu. Nataka niyaanike hapa fasta tuanze mjadala huu rasmi.

Kuna wale ambao wanaamini yakwamba, muimbaji anacho hitaji ili kua msanii au kuitwa msanii, ni nguo nzuri (umaridadi), track na video kali na labda kiki la nguvu ili apae anga za tasnia ya muziki kilaini. Lakini sio kuimba.  Hiyo haina ulazima.

Kundi hili ni la watu ambao wanategemea kubebwa na studio. Yaani, mategemeo yao yote ni kwa yule producer ataeweka auto-tune kama zote ili kujaribu kuficha ukweli kwamba sauti ya kuimba hawana.

Sasa basi, ukija jukwaani, kwa wao umuhimu ni show la kibabe na pamba kali lakini kuimba hamna kitu pale, ni sifuri. Lakini tambua kwamba kundi hili la wasanii hawajali kabisa kwamba hawajui kuimba na wala nafsi zao haziwasuti. Wao wanaona kuishi kama msanii katika mazingira haya ni jambo la kawaida kabisa na linakubalika, na haina haja kujiendeleza kama muimbaji. Yaani, kwake yeye kujihusisha na mambo haya ni kujipotezea muda tu.

Sasa tuangalie kundi hilo lingine.

Kundi hili ni wasanii au waimbaji ambao kwa kweli hawaridhiki kabisa na uimbaji wa hovyo. Ni kwamba wanashindwa wafanye nini ili kubadili hiyo hali. Ni jambo ambalo linawakera kiasi ambacho wanaona aibu kabisa kujinadi kama wasanii, nafsi zao zinawasuta. Wanajihisi kama wao ni wasanii bandia. Kundi hili ni watu ambao wakipata fursa ya kufundhishwa kuimba watafanya lolote lile ili kuboresha uimbaji wao, na hawakati tamaa. 

Je, katika haya makundi mawili, wewe ni yupi?

Natumaini makala yangu ya leo imekufurahisha kwa namna moja au nyningine. Kama umenufaika na ungependa wengine nao wanufaike, basi naomba sambaza! 

Je, ungependa kujifunza kuimba?

Kama ungependa kuanza mafunzo ya kuboresha sauti yako ya kuimba, unaweza kuanza kwa kusoma na ku-download mazoezi ya sauti na muongozo wa kina kupitia makala yangu Msaada wa Mafunzo ya Sauti na JOETT WhatsApp na Telegram.


***

JOETT - Got U On My Mind

No comments:

Post a Comment