Saturday, April 11, 2020

Mazoezi ya Sauti, na Jinsi ya Kujipatia Msingi Mzuri na Mwalimu


Kujifunza kuimba kwa kutumia program zangu nilizopandisha Mkito; au kwa kutumia program ninazo stream Tumblr; au ninazorusha kwenye WhatsApp group zangu Joett Voice Studio na Gonga Jiwe for Joett, ni njia moja wapo ya kujifunza kuimba nyumbani kwako, mradi ufuate mungozo wangu na ushauri ninaoutowa kwenye makala zangu, na pia kwa kuzingatia mifano ya video nilizopandisha Facebook; na pia kuna video yenye mifano ya Joett Vocal Drills Vol. 1-4 (bofya hapa).

Kuna watu wanaonifuata Inbox na kuniambia kwamba wanashindwa kujifunzia nyumbani. Hii hali nnaielewa sana, lakini kama unataka kujifunza bila ya gharama yoyote, basi hauna budi kujitahidi pole pole hadi uweze kufanikiwa.

Sitaki kumdanganya mtu. Kuna watu ambao nimekutana nao ndani ya studio yangu baada ya wao kujaribu mazoezi yangu nyumbani kwa muda mrefu... miezi, hata mwaka na zaidi, ambao nilipowasikiliza walikua ni kama watu hawajawahi kufanya mazoezi ya sauti hata siku moja.

Na nilipo kaa nao kufanya tathmini tu ya sauti zao (huduma ya bure), niliweza kuwaweka sawa haraka sana, ndani ya muda wa dakika 30 tu, ambapo walikua wamepambana nyumbani kimakosa kwa muda mrefu bila ya mafanikio.

Watu hutofautiana katika kujifunza. Hata wale ambao nimekutana nao katika mazingira hayo hayo na walikua wamepiga hatua kubwa, wao pia kwa darasani mwangu niliweza kuwapeleka mbali zaidi.

Sababu ya mimi kutoa mazoezi ya sauti kwa njia ya mtandao lengo langu ni kuwasaidia waTanzania wenzangu kupata angalau uelewa, na mazoezi stahiki ili waweze kujiendeleza bila swala la gharama kua ndio kikwazo kwao.

Hivyo basi, mazoezi ya ana kwa ana ya kulipia yapo, japo ni watu wachache sana ambao wapo tayari kulipia mafunzo ya aina hii... hususan madarasa ya kujifunza muziki, iwe: sauti, guitar, kinanda na kadhalika.

Hii ndio hali halisi ilivo kwa hapa Tanzania.

Kwa sisi waalimu, ni kazi ambayo bila ya kujitolea tu kuwasaidia wanaotaka kuendeleza vipaji vyao, hii elimu itakua ni ngumu sana kuifikisha kwa walengwa.

Ningependa kurudia tena, kama kuna mtu yoyote ambae ana hisi angependa kupata msingi mzuri kwa kupitia madarasa ya kulipia, basi ni vyema awasiliane na mimi kwa njia ya simu au WhatsApp.

Kwa wale ambao mpo ndani ya WhatsApp groups Joett Voice Studio na Gonga Jiwe for Joett, jaribu kuwasiliana na Admin wangu wa hizo group, Hance Mligo, (bofya hapa) ili kupata utaratibu wa madarasa kwa njia ya simu (voice call) kupitia WhatsApp na Skype.


Wewe ndie chombo halisi, jifunze kuimba kama pro! 


JOETT - Mwalimu wa Sauti 
No comments:

Post a Comment