Thursday, April 9, 2020

Lady Jaydee na Joett Wanakuletea "Vokoz" Kuelimisha Waimbaji


PRESS RELEASE -- Kipindi kipya cha Vokoz kimeanzishwa na Lady Jaydee na Joett kwa madhumuni ya kuwasaidia vijana na wasanii chipukizi wa Tanzania na East Africa kufikia malengo yao katika swala zima la kujifunza uimbaji bora.

Mlolongo wa hili zoezi uko kama ifuatavyo.

Mwalimu wa sauti Joett anatoa tathmini ya sauti ana kwa ana, kwa wote ambao wamechaguliwa kuonana nae baada ya kutuma kwa Lady Jaydee kupitia DM ya akaunt yake Instagram, historia yao fupi ya kimuziki pamoja na sauti wakiimba.

Baada ya tathmini ya sauti, Lady Jaydee na Joett watakaa kikao kuamua nani wamuendeleze kwenye mafunzo hayo ya sauti ya ana kwa ana.

Baada ya mafunzo kwa kipindi cha takriban madarasa 10, Lady Jaydee atakaa na baadhi ya hawa wanafunzi ili kuwasaidia katika utunzi wa mashairi na kurekodi nyimbo studio.

Baada ya kurekodi nyimbo Lady Jaydee atachagua nani ampe nafasi ya kufanya show na yeye kwenye jukwa lake maalum la 20th Anniversary ya Lady Jaydee.

Unaweza kuangalia Vokoz Episode 1, 2, 3 & 4 hapa chini. Kumbuka ku-Subscribe YouTube Channel ya Lady Jaydee ili uweze kufuatilia vipindi vijavyo.Subscribe YouTube channel ya Lady Jaydee, bofya hapa!

Ushuhuda wa Faida ya Mafunzo ya Sauti

Kwenye swala hili zima la uimbaji natumaini mngependa kufahamu, je sauti inaweza kufunguka au kubadilika kwa kiwango gani?

Sasa basi, ili kuwapa uelewa zaidi kuhusu faida ya mafunzo ya sauti kwa muimbaji, angalia video zifuatazo za mwanafunzi wa Joett ajulikanae kwa jina la kisanii kama Japhy Ross.

Japhy Ross, mkazi wa Mwanza, kabla ya mazoezi ya sauti alirekodi wimbo "Angejua" jijini Mwanza. Sikiliza video clip fupi ifuatayo.Baada ya masaa 10 darasani na Joett, Japhy Ross alirekodi upya wimbo "Angejua" pale Wanene Studio, Dar es salaam. Sikiliza video clip fupi ifuatayo.


Baada ya miezi 10 darasani na Joett, Japhy Ross alirejea Mwanza
 na kurekodi wimbo mpya "Unanifaa". 
Sikiliza video clip fupi ifuatayo.


MAZOEZI YA SAUTI KWA WOTE

Kwavile nafasi ni chache katika zoezi hili la Vokoz, na kwavile madhumuni ya zoezi hili ni kutoa elimu kwa wote, tungependa kukaribisha wote ambao wangependa kuboresha uimbaji wao, wajiunge na huduma ya Joett ambayo inatolewa  bila gharama kupitia mtandao.

Yaani hapa utakutana na group lake la WhatsApp na pia utaweza ku-download mazoezi ambayo amepandisha Mkito pamoja na ku-stream mazoezi aliyopandisha Tumblr.

Ili kupata maelezo zaidi tafadhali soma makala yake: "Unahitaji Mazoezi ya Sauti? Download Joett Vocal Drills Vol. 1-7!"

Natumaini kwa namna moja au nyingine mmenufaika na yaliyomo kwenye hii blog post. Tunawaomba mjisikie huru ku-share.


Wewe ndie chombo halisi, jifunze kuimba kama pro! JOETT - Mwalimu wa Sauti

Makala Zifuatazo ni Muhimu Kusoma (bofya links)

Unahitaji Mazoezi ya Sauti? Download Joett Vocal Drills Vol. 1-7!
Msaada wa Mafunzo ya Sauti na JOETT WhatsApp na Telegram
Je, Binadamu Anaimbia Tumboni? Jua Ule Ukweli Wenyewe Halisi
Jifunze Kuimba na Joett Darasani na Online: Muongozo na Utaratibu
Jifunze Kuimba: Umuhimu wa Kuelewa Madhumuni Ya Mazoezi
Jifunze Kuimba: Tatizo La Pumzi na Jinsi Ya Kulitatua
Kujifunza Kuimba Kwa Kupiga Makelele Hakusaidii Lolote
Jifunze Kuimba na Joett Mkito.com Vol. 1: Madhumuni ya Lip Rolls
Je, Utajuaje Kama Unakosea Katika Mazoezi Ya Sauti ?
Jiunge na Darasa Moja La Kukusaidia Ukae Sawa na Mazoezi Ya Sauti


No comments:

Post a Comment