Thursday, June 29, 2017

Jiunge na Darasa Moja La Kukusaidia Ukae Sawa na Mazoezi Ya Sauti

Ili kufikisha huduma yangu ya mafunzo ya sauti bila gharama, nilitengeneza na kupandisha program za mafunzo Joett Vocal Drills Volume. 1-7 Mkito.

Pamoja na hayo, kwa baadhi yenu kujifunzia na program hizo bado mnakua mnahitaji muongozo.

Nilichokifanya ni kuwapandishia video za darasani mwangu mara kwa mara kwenye Instagram yangu @joettmusic ili muweze kuona mifano, na vile vile kuna video nyingi tu kwenye channel yangu ya YouTube.


Na sasa nimeamua kufungua darasa kwa mafunzo ya lisaa limoja tu ndani ya studio yangu, ili kuwasaidia wale wanaotaka kukaa darasani na mimi kwa lisaa limoja tu, waweze kupata uelewa zaidi wa jinsi ya kufanya haya mazoezi ili wapate mafanikio ya haraka zaidi. Huduma hii inaanza mara moja.

Kama ungependa kujiunga, tafadhali nitumie ujumbe WhatsApp nikupe utaratibu.

Je, ungependa kusoma Nakala Nyeti za Mazoezi na Maelekezo ya Uimbaji Bora? Bofya hapa!

Ahsanteni!

JOETT
Vocal Coach
YouTube Channel
Madarasa Ya Studio

No comments:

Post a Comment