Wednesday, June 28, 2017

Je, Utajuaje Kama Unakosea Katika Mazoezi Ya Sauti ?


Mazoezi yangu ya sauti, yaani Joett Vocal Drills Vol. 1-4 yana madhumuni moja tu. Kuondoa tabia ya kupiga makelele na kuimbia kooni. Kwa maana nyingine, kama wewe unaimbia kooni na unapata shida kupanda na kushuka na vile vile unaumia unapo imba nyimbo, basi maana yake ni kwamba wewe hauna mpangilio stahiki wa kuimba.

Hivyo basi, unahitaji kufanya mazoezi stahiki ya sauti ili kurekebisha sauti yako uweze kuimba kwa kutumia mfumo mpya, ambao hauumizi koo wala hauchoshi sauti yako. Na juu ya hapo, mfumo huu wa mazoezi ya kuimba utakuwezesha wewe kuimba kwa upeo mkubwa na kwa urahisi kabisa.

Ukisha download Vol. 1-7 ntahitaji kusikia voice note yako ukiyafanya mazoezi ili nikupe muongozo zaidi. Usifanye Vol. 5-7 mpaka sauti imekaa sawa na mazoezi ya Vol. 1-4. Jipe muda wa wiki kadhaa. 

MUHIMU

Usilazimishe notes na wala usiimbie kooni katika training. Na tafadhali fuata piano na uimbe ndani ya funguo (key). Kuna video ya maelekezo ya Joett Vocal Drills Vol. 1-4 kwenye ukurasa wangu wa Facebook (bofya hapa). Itakupa uelewa zaidi.

Sasa basi, kama unafanya mazoezi ya Vol. 1-4 na unashindwa kuenda na funguo (key) bila ya kupiga kelelele na kujiumiza koo, basi ujue unakosea. Wacha mazoezi mara moja alafu niombe mimi ushauri kupitia WhatsApp (namba ipo kwenye bango hapo juu).

ONYO: Ukiendelea kubamiza sauti, utaua kabisa sauti yako. 

KUMBUKA: Mifano ya jinsi ya kufanya mazoezi kifasaha na bila shida yeyote wala kutumia nguvu, yapo kwenye ukurasa wangu wa Facebook (bofya hapa).

Tafadhali Soma Nakala Nyeti za Mazoezi na Maelekezo ya Uimbaji Bora. Na kama ungependa nikuweke sawa, natoa madarasa ya lisaa limoja ana kwa ana ndani ya studio yangu, Oysterbay. Kwa maelekezo zaidi, bofya hapa!


JOETT
Vocal Coach
Madarasa Ya StudioNo comments:

Post a Comment