Friday, December 2, 2016

Jifunze Kuimba na Joett Darasani: Muongozo na Utaratibu Maalum

Ukitaka kujifunza kuimba ndani ya darasa langu studio, ana kwa ana, utaratibu ni kama ufuatavyo.

Kwanza kabisa, mimi ninafundisha siku 3 tu kwa wiki… Jumatatu, Jumanne na Jumatano, na ninachukua wanafunzi wachache sana kwa siku, kwasababu ninafundisha mtu mmoja mmoja tu kila lisaa kwa kufuata ratiba iliopangwa maalum. Kwahivyo nafasi za kuchukua wanafunzi wapya huaga ni adimu sana.

Program Zangu Za Mafunzo ya Sauti  ndani ya studio yangu katika mfumo wa Speech Level Singing Comprehensive Courses zipo kama ifuatavyo: Level 1, Level 2, Intermediate, Advanced, Pro, Pro 2 na Pro Club... na kila programu ni ya masaa 10. (Yaani, kila utakapokuja darasani utafanya mazoezi kwa lisaa limoja tu). Ada ni Shilingi 310,000.

Quick Start Program 

Program ya Quick Start ni ya maandalizi na ni kwa gharama nafuu ya Shilingi 90,000, kukuwezesha wewe kwenda kufanya mazoezi mwenyewe nyumbani, na program hii ni ya masaa 3 tu ndani ya studio yangu.

1 Hour Vocal Training Session ni darasa la lisaa limoja tu kwa wale ambao wameshapitia msingi mzuri katika madarasa yangu ya ana kwa ana; na vile vile kwa wale wanaojifunza kupitia programu zangu za Jifunze Kuimba Na Joett Vocal Drills zinazopatikana Mkito.com. Darasa ilo limoja limoja linaweza kua kama nyongeza au "brush-up" ya mara kwa mara katika kujifunza kwako kuimba. Ada ni Shilingi 31,000.

VOICE ASSESSMENTS (Ukaguzi wa Sauti)

Kabla haujaanza mafunzo ya ana kwa ana, nakukaribisha uje studio kwa dakika 30 tu niskie sauti yako, na vile vile nikupitishe kwenye mazoezi kadhaa kwenye kinanda ili niijue sauti yako na changamoto zako za kurekebisha.

Hua nafanya assessments—yaani ukaguzi wa sauti, kwa wanafunzi wanaotaka kujiunga na madarasa yangu ya masaa 10—siku za Jumamosi kwa nusu saa bila gharama yeyote--ni bure, lakini kwa mihadi maalum ya muda wa assessment. Ili kupata nafasi ya assessment, tafadhali wasiliana na mimi kwa njia ya simu au kupitia WhatsApp.

DOWNLOAD TRAINING MKITO.COM

Jifunze kwa urahisi na kwa gharama nafuu ya Shs 250 tu, kwa ku-download program zangu nilizoandaa na kupandisha Mkito.com kwa ajili yako.

Kupitia mfumo huu, nimeboresha mazoezi maalum ya sauti kwa kufuata mahitaji muhimu katika kujifunza kuimba kupitia mtandao. Ili kuingia katika mstari stahiki wa mafunzo ambao bila shaka, utakuletea mafanikio ya haraka, ni vyema kuanza safari yako ya kujifunza kuimba hapa.

Na vile vile unaweza kupata maelekezo zaidi kwa kubofya nakala kadhaa nilizo andika hapa chini. Ukiwa na maswali, tafadhali jisikie huru kuniuliza. Ni muhimu sana kuelewa, na sio kufanya vitu kwa hisia bila muongozo panapo stahili. Tafuta ushauri!

Jifunze Kuimba: Umuhimu wa Kuelewa Madhumuni Ya Mazoezi

Wewe ndie chombo halisi, jifunze kuimba kama pro!


JOETT
Vocal Coach 


No comments:

Post a Comment