Tuesday, December 20, 2016

Volume 1, 2 & 3 Jifunze Kuimba na Joett Mkito.com

Je, ungependa kujifunza kuimba  kwa dhati? Basi suluhu ni kufanya mazoezi ya sauti kama nilivyowaandalia na kuwapandishia Mkito.com. Hadi sasa Volume 1, 2 & 3 zimepanda Mkito. Bado kuna Vol.  4, 5, 6 & 7 zinakuja.

Mii / Mia / Nay kwenye Volume 2 ni mwanzo wa kuanza kuunganisha irabu katika mazoezi yako ya sauti. Ukishakua mzoefu katika hilo, unaweza kufanya irabu moja moja na scale hizo hizo kwa kufanya AAA pekeyake, au EEEE pekeyake, IIII pekeyake, UUUU pekeyake, OOO pekeyake. Ukiona sauti inaingia kooni, wacha papo hapo. Jua unakosea. Endelea na lip rolls, tongue trills, MII, MIA na NAY mpaka sauti yako ikae sawa.

Lakini jua kwamba kila toleo ni muendelezo wa toleo liliopita. Utaratibu wa mazoezi mpaka toleo hili la 3 upo kama ifuatavo:

1. Pumzi
2. Volume 1
3. Volume 2
4. Volume 3

Na sasa nikupe muongozo wa Jifunze Kuimba na Joett Vocal Drills Volume 3

Mazoezi ya Vocal Drills Volume 3 ni muendelezo wa Vol. 2. Kwa mara nyingine tena, fuata maelekezo. Kama unayo maswali ama kuna kitu kinakushinda, tafadhali uliza. Nitaweza kukupa ushauri. Lakini cha msingi nikufuata maelekezo na kufanya mazoezi stahiki kama nilivowaandalia hapa. Download Volume 3 hapa!

Ukishaweza haya mazoezi ambayo muda wake ni takriban dakika 5, unatakiwa kuunganisha Pumzi, Vol. 1, 2 & 3 katika ratiba yako ya mazoezi ya sauti ya kila siku.

Na vile vile unaweza kupata maelekezo zaidi kwa kubofya nakala kadhaa nilizo andika hapa chini. Ukiwa na maswali, tafadhali jisikie huru kuniuliza. Ni muhimu sana kuelewa, na sio kufanya vitu kwa hisia bila muongozo panapo stahili. Tafuta ushauri!

Jifunze Kuimba: Umuhimu wa Kuelewa Madhumuni Ya Mazoezi
Jifunze Kuimba: Tatizo La Pumzi na Jinsi Ya Kulitatua
Jifunze Kuimba na Joett Mkito.com Vol. 1: Madhumuni ya Lip Rolls
Jifunze Kuimba na Joett Mkito.com: Vocal Drills Volume 2

Wewe ndie chombo halisi, jifunze kuimba kama pro!


JOETT
Vocal Coach
YouTube Channel
FaceBook Videos

No comments:

Post a Comment