Tuesday, December 6, 2016

Jifunze Kuimba na Joett Mkito.com: Vocal Drills Volume 2


Volume 2 ni muendelezo wa Vol. 1. Kwa maana ni lazima ufanye Vol. 1 kabla haujafanya Vol. 2. Kwa mara nyingine tena, nita sistiza mfuate maelekezo kama yalivo kwenye toleo hili. 

Mazoezi haya yana dakika 7. Ukishaweza kufanya haya mazoezi, sasa utakua na mazoezi mawili. Yaani Vol. 1 & 2 katika ratiba yako ya mazoezi ya sauti ya kila siku; na utatakiwa kufanya yote kwa pamoja kufuata mlolongo huo huo wa Vol. 1 kuingia Vol. 2.

Kumbuka, madhumuni ya haya mazoezi ni ku re-balance sauti yako, au kurekebisha matumizi ya sauti yako ili uweze kuimba kwa urahisi kwenda juu na kwenda chini; na mpangilio na ratiba hii ndio itaweza kukupa wewe huo uwezo kwa njia ya haraka na salama zaidi. Tafadhali usianze kukurupuka na ku-download vitu olela kwenye internet. Tafadhali fuata maelekezo yangu na mazoezi niliokuandalia ili uweze kupata mafanikio ya uhakika. Download Volume 2 hapa!

Na vile vile unaweza kupata maelekezo zaidi kwa kubofya nakala kadhaa nilizo andika hapa chini. Ukiwa na maswali, tafadhali jisikie huru kuniuliza. Ni muhimu sana kuelewa, na sio kufanya vitu kwa hisia bila muongozo panapo stahili. Tafuta ushauri!

Jifunze Kuimba: Umuhimu wa Kuelewa Madhumuni Ya Mazoezi
Jifunze Kuimba: Tatizo La Pumzi na Jinsi Ya Kulitatua
Jifunze Kuimba na Joett Mkito.com Vol. 1: Madhumuni ya Lip Rolls

Wewe ndie chombo halisi, jifunze kuimba kama pro!


JOETT
Vocal Coach
YouTube Channel

No comments:

Post a Comment