Friday, December 2, 2016

Jifunze Kuimba na Joett Darasani na Online: Muongozo na Utaratibu

Ukitaka kujifunza kuimba ndani ya darasa langu studio, ana kwa ana au online, utaratibu ni kama ufuatavyo.

Kwanza kabisa, mimi ninafundisha siku 4 tu kwa wiki… Jumatatu, Jumanne, Jumatano na Jumamosi. Na pia ninafundisha mtu mmoja mmoja tu kila lisaa kwa kufuata ratiba iliopangwa maalum.

Program Zangu Za Mafunzo ya Sauti  ndani ya studio yangu katika mfumo wa Speech Level Singing Comprehensive Courses zipo kama ifuatavyo: Level 1, Level 2, Intermediate, Advanced, Pro, Pro 2 na Pro Club... na kila programu ni ya masaa 10. (Yaani, kila utakapokuja darasani utafanya mazoezi kwa lisaa limoja tu).

Quick Start Program

Program ya Quick Start ni ya maandalizi, kukuwezesha wewe kujiendeleza na mazoezi ya sauti mwenyewe nyumbani.

Kwa mfano: kama ume download Joett Vocal Drills kutoka Mkito.com na ungependa nikuweke sawa, program hii ya masaa 3 ndani ya studio yangu, ni halisia kwa ilo.

1 Hour Vocal Training Session ni darasa la lisaa limoja tu kwa wale ambao wameshapitia msingi mzuri katika madarasa yangu ya ana kwa ana; na vile vile kwa wale wanaojifunza kupitia programu zangu za Jifunze Kuimba Na Joett Vocal Drills zinazopatikana Mkito.com. 

Darasa ilo limoja limoja linaweza kua kama nyongeza au "brush-up" ya mara kwa mara katika kujifunza kwako kuimba.
TATHMINI YA SAUTI YAKO

Kabla haujaanza mafunzo ya ana kwa ana, nakukaribisha uje studio kwa dakika 30 tu niskie sauti yako, na vile vile nikupitishe kwenye mazoezi kadhaa kwenye kinanda ili niijue sauti yako na changamoto zako za kurekebisha.

Hua nafanya assessments—yaani tathmini ya sauti, kwa wanafunzi wanaotaka kujiunga na madarasa yangu ya masaa 10—siku za Jumamosi kwa nusu saa bila gharama yeyote--ni bure, lakini kwa mihadi maalum ya muda wa assessment. Ili kupata nafasi ya assessment, tafadhali wasiliana na mimi kwa njia ya simu au kupitia WhatsApp.

DOWNLOAD TRAINING MKITO.COM

Jifunze kwa urahisi na kwa gharama nafuu ya Shs 250 tu, kwa ku-download program zangu nilizoandaa na kupandisha Mkito.com kwa ajili yako.

Kupitia mfumo huu, nimeboresha mazoezi maalum ya sauti kwa kufuata mahitaji muhimu katika kujifunza kuimba kupitia mtandao. Ili kuingia katika mstari stahiki wa mafunzo ambao bila shaka, utakuletea mafanikio ya haraka, ni vyema kuanza safari yako ya kujifunza kuimba hapa.

Tafadhali, ukishindwa ku-download Mkito, wasiliana na mimi nikusaidie kupata hizo MP3 za mafunzo kupitia mfumo mwingine.

Na vile vile unaweza kupata maelekezo zaidi kwa kubofya nakala kadhaa nilizo andika hapa chini. Ukiwa na maswali, tafadhali jisikie huru kuniuliza. Ni muhimu sana kuelewa, na sio kufanya vitu kwa hisia bila muongozo panapo stahili. Tafuta ushauri!

Soma Nakala Nyeti za Mazoezi na Maelekezo ya Uimbaji Bora
Jifunze Kuimba: Umuhimu wa Kuelewa Madhumuni Ya Mazoezi

Wewe ndie chombo halisi, jifunze kuimba kama pro!


JOETT
Vocal Coach 


No comments:

Post a Comment