Tuesday, September 20, 2016

Jifunze Kuimba: Umuhimu wa Kuelewa Madhumuni Ya Mazoezi

Kabla sijaanza, ningependa kuwafahamisha yakwamba Jifunze Kuimba na Joett Vol. 1 ipo Mkito. Ni mazoezi maalum ya sauti ambayo nimeyaandaa kwa ajili yenu.

Mazoezi ya sauiti sio kuenda sehemu za wazi au Coco Beach kupiga makelele, bali ni mazoezi stahiki ya kukuza kipaji chako cha kuimba.

Mwalimu wa sauti kama mimi, ni mtu anae ielewa hii fani kwa kina, na jinsi matumizi ya sauti kwenye swala la kuimba na hata kuongea, yanavostahili kua.

Kwa ufupi: mtu yeyote anaekuambia upige makelele au uimbie puani kujifunza kuimba, atakua anakudanganya tu. Ukitaka kujua hasara za kupiga makelele maeneo ya wazi, soma Kujifunza Kuimba Kwa Kupiga Makelele Hakusaidii Lolote.

Sasa nataka nitoe maelekezo, ili uweze kuelewa kujifunza kuimba maana yake nini haswa, na vile vile ningependa uelewe kwa kina zaidi nini chakufanya ili uweze kupata mafanikio na sauti yako.

1. Mazoezi ya kuimba hufanyika na kinanda kwa mazoezi yajulikanayo kwa neno la Kiingereza, kama scales. Lakini ufanisi wake kwa kuzingatia maelekezo ndio unaoweza kukuletea wewe mafanikio.

2. La msingi nikwamba tunajaribu kuunganisha sauti yako ya kifua (yaani chest voice) na sauti yako ya kichwa (yaani head voice) kwa kupitia sauti ya kati (yaani blend)… ile sehemu ambayo sauti hizo mbili zinakutana, bila ya kuhusisha kabisa misuli ya nje ya koromelo au kwa lugha ya Kiingereza, voice box au larynx. Hiyo misuli inapoingilia katika utengenezaji  wa sauti, ndipo unaona mtu mishipa inamsimama; anapiga kelele; koo inauma; sauti inakauka; na hafiki popote.

3. Ili kufanikisha hili zoezi la kujifunza kuimba, sikiliza mifano ambayo nimepandisha kwenye Facebook yangu kwa ku bofya hapa. Lakini, hakikisha unaelewa kinachotendeka kwa kutega sikio tu na kusikiliza kwa umakini. Sikia jinsi ninavofundisha, na maelekezo ninayo yatoa kwa wanafunzi wangu. Usijaribu kufanya mazoezi na video hizi. Unaweza ukapotea vibaya. Nimezipandisha video YouTube ili kuwasaidia mmpate uelewa zaidi kuhusu swala la mazoezi ya kuimba. Kama ungependa kufanya mazoezi, soma lifuatalo hapa chini.

4. Ukishapata uelewa, unaweza ku-download Zoezi La Pumzi ambalo utafanya kabla ya kuanza Joett Vocal Drills Vol. 1 na kuendelea. Download mazoezi yangu Mkito.com.

5. Kumbuka, haya mazoezi niliyopandisha Mkito.com yatakupa msingi mzuri na kukuwezesha kuanza kujifunza kuimba popote pale ulipo bila ya kuhudhuria madarasa yangu studio. Kama ungependa kujiendeleza zaidi, basi mafunzo ya ana-kwa-ana ndani ya studio yangu ndio mpango mzima. Nimeandaa program za aina nyingi. Kuna za masaa 10, masaa 3, lisaa limoja na vile vile mazoezi ya kuimba kwa njia ya simu kwa dakika ishirini tu. Tafadhali wasiliana na mimi kama utahitaji mojawapo ya huduma hizo.

Natumaini umefaidika na maelezo hapo juu. Kama utakua na maswali yeyote, tafadhali nijulishe. 


Wewe ndie chombo halisi, jifunze kuimba kama pro!


JOETT
Vocal Coach
Madarasa ya StudioNo comments:

Post a Comment