Tuesday, April 23, 2013

Kujifunza Kuimba Kwa Kupiga Makelele Hakusaidii Lolote


Katika kazi yangu ya kufundisha kuimba, nimekutana na waimbaji wengi hapa bongo ambao hapo awali, kabla ya kukutana na mimi, walikua wana desturi ya kujifunza kuimba kwa kupiga makelele. Nimepata ripoti ya kua kuna baadhi ya kwaya ambazo hushauri wanakwaya wao kupiga kelele hadi siku ifuatayo wanakuta sauti zimakauka.

Nimepata ripoti kuhusiana na vijana wa bongo flava wanavokwenda kwenye ufukwe wa bahari kufanya mazoezi ya kuimba kwa kupiga makelele. Sii makosa yao. Kwani asiejue atafanya lolote lile analoambiwa kwa kuamini kwamba hicho kitendo kitamsaidia kua muimbaji mzuri zaidi. Hivyo ndivo jinsi wanaadamu tulivo.

Kwa mantik hiyo basi, ningependa kutoa ushauri wangu hapa, kwamba huo mwenendo potovu husababisha uharibifu wa sauti, na usipoangalia, unaweza ukawacha kuimba kabisa kwasababu kunakiwango cha uharibifu ambacho hakiwezi kurekebishika. Kwa maana ukisha fikia kiwango hicho, sahau habari za kuimba. Hutakua na sauti tena.

Ni hivi: Sauti, ili kuendana na muziki wenye mpangilio maalum kupitia kinanda, guitar na kadhalika, inatakiwa kuweza kupanda na kushuka kirahisi na bila kelele za kuumiza koo. Na vilevile, hupaswa kua na melodi yakuvutia ambayo inaendana na muziki huo.

Sasa basi, ili kuweza kufika katika levo hiyo inabidi ujifunze kuimba kufuatana na funguo (ama key) za muziki kupitia, kwanza kabisa, chombo asilia cha muziki kijulikanacho kama kinanda. Kindanda kina panga sauti yako katika njia tofauti kupitia mazoezi maalum kwa ajili hiyo, kama vile arpeggios, octaves, chromatic scales, descending scales na kadhalika. Hiyo ndio misingi ya kuimba ambayo nimepangilia katika mazoezi ninayo toa, na vile vile kwenye CD yangu Jifunze Kuimba na Joett. Kama ungependa nikupe assessment ya sauti yako, tafadhali wasiliana na mimi. Assessment za nusu saa hufanyika katika studio yangu siku za Jumamosi, na ni bure kabisa.

Ili kuanza kupata mafunzo ya bure kupitia mtandao huu, soma Jifunze Kuimba: Umuhimu wa Kuelewa Madhumuni Ya Mazoezi, na pia utawaze ku-download mazoezi yangu maalum ya sauti.

Wewe ndio chombo halisi, jifunze kuimba kama pro!


JOETT

Vocal Coach & Author "Letters from a Vocal Coach"
Private Singing Lessons
BUY Online Singing Lessons Course



No comments:

Post a Comment