Saturday, November 26, 2016

Jifunze Kuimba na Joett Mkito.com Vol. 1: Madhumuni ya Lip Rolls

Kwenye mazoezi ya Joett Vocal Drills Vol. 1 utakutana na Lip Rolls na Tongue Trills. Zote nimeelekeza jinsi ya kufanya na kutoa mifano kwenye mp3 kabla ya kuanza mazoezi hayo.

Hapa ningependa tu kutoa maelekezo kuhusu malengo ya haya mazoezi mawili.

Kwa ufupi, yana ondoa tabia ya kuimbia kooni. Unapofanya haya mazoezi misuli ilioko nje ya koromelo lako haishtuki na kukaza. Hapo basi sauti inapata urahisi wakutembea kwenda juu na chini bila ya shiriksho hilo la misuli ya kooni katika utengenezaji wa sauti.

Ukizoea hili zoezi, baada ya muda, hii tabia ya utulivu wa misuli ya nje ya koromelo lako linakufuata katika kuimba nyimbo. Kama unashindwa kufanya Lip Rolls au Tongue Trills, jaribu kufanya mazoezi haya kwa kutamka “Mmm” badala yake (yaani humming).

Muongozo wa Mazoezi

  • Download mazoezi Mkito.com
  • Weka kwenye CD au Flash Disk
  • Tumia chombo cha muziki cha kupigia CD/Flash au kama unatumia simu yako ya mkononi, hakikisha unaunganisha na speaker kupata sauti kubwa kulingana na sauti yako ukiimba. 
  • Fanya mazoezi ndani ya chumba na sio kwenye maeneo ya wazi, wala sio kwa kutumia simu yako ya mkononi na headset zake masikioni. 
  • Ku-Download PDF yenye maelekezo ya Volume 1, 2, 3 & 4 Bofya hapa!
  • Kusoma Press Release bofya hapa!

Ukiwa na maswali, jiskie huru kuniuliza, au soma nakala kadhaa nilizo andika:
Jifunze Kuimba: Umuhimu wa Kuelewa Madhumuni Ya Mazoezi
Jifunze Kuimba: Tatizo La Pumzi na Jinsi Ya Kulitatua

Wewe ndie chombo halisi, jifunze kuimba kama pro!


JOETT
Vocal Coach
Madarasa ya Studio

No comments:

Post a Comment