Thursday, November 24, 2016

Jifunze Kuimba na Joett Kupitia Mkito.com Yazinduliwa Rasmi

== PRESS RELEASE 24.11.2016 == Kwa mara ya kwanza kabisa, mtandao wa ku-download mziki wakitanzania Mkito.com, unajiunga na mwalimu mahiri wa sauti Tony Joett, kuwaletea watanzania huduma ya mafunzo ya sauti kwa wale ambao wangependa kujifunza kuimba kupitia mtandao na kwa gharama nafuu, nakupokea mafunzo yalio andaliwa kitaalamu kwa lugha ya Kiswahili na ambayo yataweletea mafanikio ya haraka na ya uhakika.

Joett ameandaa programu hizo za mafunzo ya sauti kwenye studio ya producer Lucci wa Transformax Records, ambae pamoja nae walikua majaji wa Airtel Trace Music Star Season 2 mwaka 2016. “Madhumuni ya kuandaa mazoezi haya maalum,” alisema Joett “nikuwawezesha watanzania kujifunza kuimba kwa urahisi, ili kutatua hili tatizo la vijana kuto jua pakugeukia kupata mafunzo haya ya kitaalamu na ambayo yanakuza vipaji kwa viwango vile vya kimataifa.”

Maandalizi ya programu hizi yamegawanywa katika volume ama toleo 4, ambazo toleo la kwanza ndio msingi; toleo la pili ni muendelezo; na toleo la 3 na la 4 zinaelekea kwenye viwango vya juu zaidi vya mafunzo ya kuimba, kwahivyo ili kupata mafanikio mwanafunzi atahitaji kuanzia tole la kwanza hadi kufikia la 4 na kwa mpangilio huo maalum, alafu hatimae kufanya mazoezi yote manne kwa pamoja. Kwa ujumula, mazoezi yote manne kwa pamoja yanachukua takriban dakika 30. Vile vile kuna zoezi stahiki la pumzi lililoandaliwa na Joett.

Watu wanaopenda kujifunza kuimba wataweza ku-download kila toleo kwa shilingi 250 tu, na kupata ushauri na muongozo kutoka kwa Joett kupitia Mkito.com na blog la JoettMusic.com.

Joett ambae pia hutoa mafunzo ya sauti ya ana kwa ana katika studio yake jijini Dar es salaam, ni mwalimu alie bobea kwa kipindi kirefu na anao uzoefu na utaalamu katika fani ya kufundisha sauti. Mafunzo anayotoa Joett yanasaidia kurekebisha matumizi ya sauti ili kuondoa tatizo sugu la kuimbia kooni; kupiga makelele wakati wakuimba; kuumia kooni na kukauka kwa sauti; na hujenga uwezo wa sauti ya mwimbaji kwenda juu na kwenda chini kwa urahisi na bila ya maumivu wala mateso ya aina yeyote.

Download Joett Vocal Drills Vol. 1 kuanzia alhasiri ya tarehe 24.11.2016 Mkito.com

Wewe ndie chombo halisi, jifunze kuimba kama pro!


JOETT
Vocal Coach
Madarasa ya Studio

No comments:

Post a Comment