Monday, February 26, 2018

Joett Voice Studio: Utaratibu wa Zoezi la Tathmini ya Sauti

TATHMINI YA SAUTI YAKO

Utaratibu wa zoezi hili la tathmini ya sauti ni kwa wale ambao bado hawajafika kuniona studio kwa tathmini tu.

Kwa wale ambao tayari wamesha fanyiwa tathmini na kupewa muongozo, hatua ifuatayo ni aidha kuendelea na mazoezi ya sauti nilio pandisha Mkito.com au kufanya booking ya kuanza madarasa studio. Muongozo na programu zote zipo hapa.

Madhumuni ya Assessment ni kwamba, kabla haujaanza mafunzo ya ana kwa ana, nakukaribisha uje studio kwa dakika 30 tu niskie sauti yako, na vile vile nikupitishe kwenye mazoezi kadhaa kwenye kinanda ili niijue sauti yako na changamoto zako za kurekebisha.

Sasa nafanya assessments—yaani tathmini ya sauti, kwa wanafunzi wanaotaka kujiunga na madarasa yangu ya masaa 10—siku za Jumatatu hadi Jumamosi kwa nusu saa bila gharama yeyote.

Ni bure, lakini kwa mihadi maalum ya muda wa assessment. Ili kupata nafasi ya assessment, tafadhali wasiliana na mimi kwa njia ya simu au kupitia WhatsApp.JOETT - Vocal Coach & Author:
“101 Letters from a Vocal Coach”
No comments:

Post a Comment