Saturday, October 1, 2016

Jifunze Kuimba: Irabu - Msingi wa Uimbaji Bora, Sio Ngoma Za Asili

Kila neno tunalo tamka na kuimba lina irabu au baadhi ya irabu (A E I O U), na ndio chanzo cha matatizo makubwa kwenye swala la kuimba.

Nilikua ninamshauri mwanafunzi wangu mmoja juzi kati, kuhusu chanzo cha watanzania ama waafrika kwa ujumla, kupiga makele wakiimba. Nikamwambia hivi: “ukisikiliza watu wanaimba kwenye ngoma za kienyeji unasikia kitu gani? Unasikia makelele.” Je, kunauwezekano tume rithi hilo? Sijui, lakini kiukweli dalili zipo.

Ngoma zenyewe kinachopigwa ni ngoma tupu na labda vyombo vingine vya asili, lakini vyombo hivyo havina “scale” yaani chord za kupanda na kushuka ili kutengeneza melody zinazoleta utamu na ladha katika uimbaji. Kwahivyo basi, umuhimu wa kuimba kufuatana na muziki unakua haupo. Matakoe yake, watu wanaimba kwa kupiga makelele mwanzo hadi mwisho.

Kwenye muziki ambao unatumia vyombo vya kisasa, sauti ya binaadamu pia inatakiwa kuowana na ule muziki. Ili kubadili huo mfumo wa kuimba kwa kupiga kelele (au kooni) basi, inabidi kubadili jinsi unavotumia sauti yako, kwa kufanya mazoezi maalum ya sauti ya kukuwezesha wewe kwenda na wakati na kukua kimuziki... kama muimbaji.

Kwa mifano ya mazoezi stahiki ya sauti (yaani scales), JIUNGE na YouTube Channel Yangu Leo. Bofya hapa!

Na kupata muongozo wa jinsi ya kuanza mazoezi haya kufuatana na uwezo wako wewe binafsi (kila mtu anauwezo tofauti), tafadhali wasiliana na mimi.

Wewe ndie chombo halisi, jifunze kuimba kama pro!


JOETT

Vocal Coach & Author "Letters from a Vocal Coach"
Private Singing Lessons
BUY Online Singing Lessons Course
Any Texts

No comments:

Post a Comment