Friday, April 15, 2016

Mpangilio Maalum wa Kujifunza Kuimba na Joett Kupitia WhatsApp

Nimetoa mafunzo kwa jamii bila gharama yeyote kupitia WhatsApp kwa kipindi kirefu sasa. Na changamoto zipo, ndio maana imebidi mara kwa mara kubadili mfumo ili kuboresha huduma hii.

Jambo la muhimu kabisa ni kufanya mazoezi kwa mpangilio ambao utaleta mafanikio kwako.

Kujifunza wewe mwenyewe nyumbani sio jambo rahisi. Inataka kujituma, na pia wewe mwenyewe unahitaji kutuma mazoezi yako kwangu kwa Voice Note kupitia WhatsApp, ili niweze kusikia na kutoa muongozo na ushauri.

Kama unataka kujifunza kuimba, hili jambo ni muhimu sana, kwahivyo tafadhali usipuuzie. Kwa wanafunzi wangu ambao wanalipa ada na kuja studio kwa mafunzo, kuna tofauti kubwa sana kwasababu mimi nipo hapo kusimamia kila zoezi wanalofanya.

MAANDALIZI

PUMZI ndio zoezi la kwanza na la muhimu kabisa kabla ya kufanya zoezi la sauti (yaani scales). Unaweza ku-download mp3 ya Breathing Exercise kwenye kurasa langu la Hulkshare hapa. Zingatia unafanya pumzi yako kimya kimya. Kwenye mp3 sauti ni kubwa kwasababu ya kipaaza sauti ambacho kina nasa na kukuza sauti.

ZOEZI la sauti ambalo ni muhimu kabisa kuanza nalo ni la 5 Minute Lip Rolls with Joett. Fuata maelekezo alafu ufanye zoezi hilo. Ukishaona unaliwezea, jirekodi unitumie WhatsApp nisikie na niweze kutoa ushauri. Baada ya hapo, nitakupa ushauri zoezi gani lingine ufanye ili kuboresha sauti yako. Tafadhali usikurupuke na kufanya zoezi lolote tu bila ushauri. Badala ya kujijenga, utakua unabomoa. Video ifuatayo ni mfano wa zoezi la Lip Rolls. Angalia ili uelewe jinsi ya kufanya zoezi la 5 Minute Lip Rolls with Joett kwa kutumia mp3 toka kurassa langu la Hulkshare.


UTARATIBU

Tafadhali tumia computer ku-download mp3, halafu burn kwenye CD, na baadae tumia CD player kufanyia mazoezi. Usitumie sauti ya simu wala headset ya simu kufanya mazoezi ya sauti kwasababu sauti ya simu haitoshi... kwa maana hailingani na ya binaadamu. Ni hafifu sana. Matokeo yake, sauti yako pia itakua hafifu na isiyo na mvuto wala ladha yeyote.

MIFANO

Nimeweka mifano mingi kama Joett Studio Session (for reference only), na Joett Case Study #7a kwenye kurasa langu la Hulkshare kutoka madarasa ninayotoa studio, ili kukuwezesha wewe kuelewa zaidi madhumuni ya vocal training. Sikiliza ili uelimike.

Wewe ndio chombo halisi, jifunze kuimba kama pro!

JOETT

Vocal Coach & Author "Letters from a Vocal Coach"
Private Singing Lessons
BUY Online Singing Lessons Course


6 comments:

  1. yote kwa yote nitoe shukrani sana na pongezi kubwa kwa kusaidia mpaka wasiokuwa na uwezo
    mungu ndo atakulipa kwa hili unalolifanya
    kwan mtaani tupo wengi tusiojua na tunajiona tunajua

    ReplyDelete
  2. Tariq, ahsante. Najaribu tu kusaidia. Kuhusu madarasa ya studio, kila post yangu, ukiangalia chini kabisa--chini ya juna langu, utaona link ya Private Singing Lessons. Bofya hiyo kupata info zaidi kuhusu madarasa na gharama zake.

    ReplyDelete
  3. Kwa kupitia mifano hii mungu akutunze maana nahisi nitakua sishikiki ntaweza kuimba hata kwa band mzee baba mngu akupe uhai mlefu kwani kikubwa sina cha kukupa ila ipo siku utaonja mayunda yangu

    ReplyDelete
  4. Hakika wewe ni mtu bora kati ya waliopo nchini unastajili tuzo mzee kabla sijaanza darasa lakini nina imani na wewe kwani mifamo ipo wazi ila nitakuwa mwanafunzi bora na muelewa muda wote ili baadae nijivunie kuwa na wewe na we pia ujivunie kuwa na mie katika kuleta soko la ushindani kwenye muziki wa Bongofleva

    ReplyDelete