Sunday, October 5, 2014

Msanii Chipukizi G Fullah Kwenye Singo Mpya ya Joett Afariki Dunia

Niliwasiliana na G Fullah mara ya mwisho tarehe 14 September. Nilikua ninampa taarfia kwamba yumo kwenye singo yangu mpya aki-chana, na kwamba mixing na mastering inafanywa Marekani, na akafurahi sana. Nikamwambia nitamuita wiki ifuatayo tuje kuongea zaidi kuhusu project yetu. Ile wiki ilyofuatia sikumwita. Nilibanwa sana kikazi. Nikaja kumtumia SMS tarehe 27 Septemba lakini hakujibu. Nikajaribu tena tarehe 1 Octoba, hakujibu. Nikapiga simu mara kibao, hapatikani.

Jana jioni nilikua na video producer wangu Meja tukijadili mikakati ya kutengeneza video, nikamwambia Fullah kapotea. Sijui yuko wapi. Nilikua na hofu sana.

Cha ajabu, asubuhi ya leo napata habari ya kwamba mwenzetu amefariki leo asubuhi, na kwamba alikua anaumwa sana. Nimetoka kuongea na shemeji yako hivi punde, na kaniambia wanaterajia kumzika kesho. Kwao wanapoishi familia yake na palipo msiba ni Mbezi Beach.

Ni pigo kubwa sana. Kama mwalimu wake na msanii
wangu kwenye lebo yangu Joett Music, nimehuzunishwa sana na kifo cha G Fullah. Singo yangu mpya ambayo nimemshirikisha yeye pamoja na vijana wa Level One (ambao pia ni wasanii wangu), tunaiachia rasmi Octoba 13, na nimeamua kwamba nita dedicate the video to him. Tunaterajia ku-shoot baada ya wiki kadhaa, na mapaka hapo tutakapokamilisha zoezi hilo, nina muomba mungu atupe nguvu katika wakati huu mgumu. Fullah alikua ni mtu mzuri, mkarimu na mwenye subra na upendo kwa jamii iliomzunguka. Nawapa pole wanafamilia, ndugu na marafiki zake wote. Mola ailaze roho yake pema peponi.

Sikiliza Audio YouTube I'm Gonna Live Forever by Joett (ft. G Fullah & Level One) 

JOETT

No comments:

Post a Comment