Thursday, July 18, 2013

Jinsi Halisi ya Kupumua, Kuimba na Kumudu Sauti [VIDEO]

Kuimba kunahitaji pumzi kwasababu pumzi ndio itakayo kuwezesha kumudu ile sauti na kuipeleka popopote pale unapotaka. Bila "control" sauti yako itakua hafifu na isiyo na mvuto wala. Kwa hivyo basi, nimeanda video fupi ya kama dakika tano hivi, ili kukuonyesha jinsi ya kupumua na wapi kupumua (kabla ya kila mstari); na ukiangalia video vizuri utaona jinsi ya kumudu sauti yako na kuongeza kasi na ujazo wenye ladha ya kuvutia. Kwa maelekezo zaidi angalia video Jifunze Kuimba na Joett: Jinsi Halisi ya Kupumua, Kuimba na Kumudu Sauti.

Kama unamaswali na ungependa nikutengenezee video maalum kukusaidia wewe kusawazisha ama kurekebisha linalo kushinda ama linalokupa matatizo kwenye kuimba, wasiliana nami. Namba zangu za simu na barua pepe zipo hapo juu, na vile vile, naweza kupatikana kwa kupitia SKYPE ambapo ID yangu ni tojona. Mafunzo ya kuimba ni muhimu sana kama unataka kuwa na uwezo wa juu katika fani hii. CD yangu yakufundishia inaweza kukusaidia. Mpaka hapo siku nyingine, nakutakia siku njema!JIFUNZE KUIMBA NA JOETT VOCAL TRAINING CD PACKAGE

Package inakupa CD singo 3 za Joett BURE (Color Me Beautiful, I Could Never Live (Without Your Love), Heaven Said) pamoja na instrumeto zake. Kama upo Dar es salaam, unaweza kuja nikupe ushauri BURE na kukuonyesha jinsi ya kuitumia CD yangu yakujifundishia vyema. Na pia unaweza kununua Jifunze Kuimba na Joett kwenye intaneti. Kama upo Dar unaweza kuja nunua na kuchukua kwenye studio yangu Oysterbay. Bei yake ni TShs 35,000/=.

Wewe ndio chombo halisi, jifunze kuimba kama pro!

JOETT
Vocal Coach & Author
Private Singing Lessons
Letters from a Vocal Coach
Learn to Sing with Joett Vocal Training CD
BUY Learn to Sing with Joett CD Online from TripleClicks

Download Joett tracks from iTunes, Amazon MP3, TuneCore.
Buy Joett CDs from A Novel Idea Bookstores Dar, Zanzibar, Arusha.
Nationwide CD distribution via Joett Music (Airtel Money, TIGO Money, M-Pesa).
Follow me on Twitter
Become a fan on Facebook 
Follow Joett On Facebook

No comments:

Post a Comment