Friday, May 15, 2020

Mazoezi ya Sauti LIVE kwa Njia ya Simu Unaporekodi Ngoma Studio

Mara nyingi producer ndani ya studio atakua na changamoto nyingi wakati wa kumrekodi msanii.

Na changamoto hizi zinatokana na sauti ya muimbaji kutokidhi viwango vinavyohitajika kutengeneza ngoma nzuri.

Kutoka kipindi chetu cha #Vokoz, sasa tunawaletea mazoezi ya sauti ndani ya recording studio kwa njia ya simu ili kutatua matatizo ya sauti ya muimbaji papo kwa hapo.

Tunakaribisha recording studios popote Tanzania ambao wangependa msaada wa vocal training ya papo kwa hapo kwa njia ya simu, ili kurekebisha sauti wakati wasanii wapo ndani ya studio wana rekodi ngoma.

Hii huduma ya majaribio ni BURE na ni muendelezo wa kipindi cha #Vokoz cha Lady Jaydee na Joett. UTARATIBU - #VOKOZ LIVE


Nahitaji information zako, yaani Jina Kamili, Umri, Namba ya Simu, anuani yako ya Barua Pepe. Hii chart nitaijaza mimi kwa kalamu hapa studio na itakua ndio faili yako.

Vocal Coaching                                                 Sessions Log

Name_______________________      Age______      Mobile #

Email_______________________


Date
Start Time
Vocal Exercise
Session Duration
SignatureSTEP 1:  Download Skype app. (WhatsApp sio mbaya lakini Skype ni bora zaidi).

STEP 2: Hakikisha simu yako imeunganishwa na spika (external speakers) kama speaker ya bluetooth au home theater, ili uweze kusikia sauti ya kinanda kama ilivyo.

STEP 3: Zoezi la Pumzi (ntarusha awali ujiandae kabla).

STEP 4: Tathmini ya tatizo la sauti

STEP 5: Tutaanza mazoezi kwa njia ya simu kwa kutumia VOICE CALL (sio video call)


VIFAA NYONGEZA

Ukiwa na device nyingine moja, yaani smartphone, tablet au computer, nitaweza kukurushia mazoezi ambayo ntatengeneza na kurusha ili uweze ku-play kwenye speaker huku tupo kwenye simu nikisikiliza ukifanya mazoezi.

IGTV

Huduma hii ni bure lakini tungependa recording studio ifanye ku-stream LIVE IGTV matukio ya ndani ya studio, kama itawezekana, ili kuhamasiha na wengine.

Tag: @vokoztz @joettmusic @jidejaydee


JOETT - Mwalimu wa Sauti

No comments:

Post a Comment