Thursday, January 12, 2017

Jifunze Kuimba na Joett Mkito.com Vol. 5

Tarehe 17, Jan toleo la tano la Joett Vocal Drills lina drop Mkito.com. 

Natumaini mpaka sasa mtakua mmesha download na kufanya mara kwa mara Zoezi La Pumzi, Vol. 1, 2, 3 & 4.

Jinsi pekee ya kukuza kipaji chako ni kufanya haya mazoezi mara kwa mara... angalau mara 3 kwa wiki. Tafadhali zingatia hilo. Ni muhimu sana.

Sasa katika toleo hili la tano, muda muafaka umewadia kutumia sauti yako ulio ijenga katika mazoezi, kuimba wimbo Color Me Beautiful pamoja na guitar.

Nimegawa mashairi kwa mistari ili uweze kufanya zoezi na sauti kwanza kabla ya kuimba na guitar pekeyako.

Mashairi kwa zoezi hili yapo hapa chini. 

"Joett - Color Me Beautiful" [Lyrics]

You make the world a better place
Your love is divine, straight down the line
Take me away from what I know
Onto a better place
There in your arms
Your love is divine, straight down the line

Cos you know that I’m addicted to love
Cos you know that I’m addicted to love
So color me beautiful
Color me blind

Muongozo wa Mazoezi

• Download Mazoezi Mkito.com
• Weka kwenye CD au Flash Disk
• Tumia chombo cha muziki cha kupigia CD/Flash au kama unatumia simu yako ya mkononi, hakikisha unaunganisha na speaker kupata sauti kubwa kulingana na sauti yako ukiimba.
• Fanya mazoezi ndani ya chumba na sio kwenye maeneo ya wazi, wala sio kwa kutumia simu yako ya mkononi na headset zake masikioni.

Na vile vile unaweza kupata maelekezo zaidi kwa kubofya nakala kadhaa nilizo andika hapa chini. Ukiwa na maswali, tafadhali jisikie huru kuniuliza. Ni muhimu sana kuelewa, na sio kufanya vitu kwa hisia bila muongozo panapo stahili. Tafuta ushauri!

Jifunze Kuimba: Umuhimu wa Kuelewa Madhumuni Ya Mazoezi
Jifunze Kuimba: Tatizo La Pumzi na Jinsi Ya Kulitatua
Jifunze Kuimba na Joett Mkito.com Vol. 1: Madhumuni ya Lip Rolls
Jifunze Kuimba na Joett Mkito.com: Vocal Drills Volume 2
Volume 1, 2 & 3 Jifunze Kuimba na Joett Mkito.com
Jifunze Kuimba na Joett Mkito.com: Vocal Drills Volume 4


Wewe ndie chombo halisi, jifunze kuimba kama pro! Nawatakia mafanikio mema!


JOETT
Vocal Coach
YouTube Channel
Madarasa ya Studio

No comments:

Post a Comment