Wote tunaelewa na kukubali manufaa ya teknolojia katika maisha yetu. Leo ningependa kugusia jinsi ambavo utaweza kujifunza kuimba kwa kutumia simu yako ya mkononi. Tunatumia simu zetu kuangalia video; kusikiliza muziki; kwenye mitandao ya kijamii bila matatizo kabisa, lakini ili kujifunza kuimba kupitia simu ya mkononi tunahitaji vitu kadhaa ili kuweza kukamilisha zoezi la mafunzo.
Kwanza kabisa, sauti yako inatakiwa iendane na sauti ya kinanda kwa usawa. Sio kinanda kiko chini kwa kutumia speaker ya simu pekeyake au headphone za simu. Ni muhimu sana uweze kusikia sauti yako, na vile vile kusikia sauti ya kinanda ambayo inalingana na sauti ya binadamu. Kwahiyo, kimsingi unahitaji kukamilisha hilo. Na jinsi ya kukakamilisha jambo hilo utahitaji kuunganisha simu yako kwenye home theater au boom box.
JINSI YA KUJIFUNZA KWENYE SIMU
Mimi nitakua kwenye kinanda ambacho kitakua
kimeunganishwa kwenye speaker za home theater yangu studio, ili wewe uweze kusikia kinanda vizuri kupitia simu yangu. Upande wako pia, unahitaji kutumia home theater au boom box ambayo nayo imeunganishwa na simu yako, ili usikie sauti kubwa na yakutosheleza kama vile nilivoelekeza hapo juu. Utakapo imba zoezi nitakazo kupa, sauti yako pamoja na kinanda zitanifikia mimi kupitia simu yako ya mkono kwenda kwenye simu yangu mimi ambayo itakua inapaazwa na speaker za boom box yangu. Kwahiyo kwa kifupi, kazi ya mafunzo inaweza ikaenedelea vizuri—kama vile upo ndani ya studio yangu.
ADA YA DARASA
Kujiunga na mafunzo, utahitaji kunipigia simu au kuwasiliana nami kwa njia yeyote. Ada kwa darasa moja la dakika 20 ni Shilingi 12,000 na malipo yake ni kupitia namba yangu ya Tigo Pesa ambayo ipo kwenye kipeperushi changu cha rangi nyekundu na nyeupe hapo juu.
SALIO KWENYE SIMU
Ni muhimu uwe na salio kwenye simu lakukuwezesha kukaa hewani kwa muda wa dakika ishirini kwa kutumia simu ya kawaida. Simu kupitia WhatsApp au Viber inatatizo la kukata mara kwa mara, na vile vile, ikiingia simu ya kawaida hukata kabisa. Kuepuka usumbufu bora kutumia simu ya kawaida. Ukijiunga na vifurushi stahiki, huduma hii ina bei nafuu mitandao yote nchini Tanzania. Karibuni kujifunza kuimba kupitia simu yako ya mkononi, kuanzia tarehe 1 Februari, 2016.
"Wewe ndio chombo halisi, jufunze kuimba kama pro!"
JOETT
Vocal Coach & Author "Letters from a Vocal Coach"
Private Singing Lessons
BUY Online Singing Lessons Course
No comments:
Post a Comment