Friday, September 16, 2011

Chungu Kimechemka TIKISA: Madansa Wapandisha Gemu

Vijana wa TIKISA wanatisha.Wiki iliopita nilikua najiuliza, "hawa watu mbona wananichanganya?" Manake gemu limepanda hadi sisi majaji (Joett, QSK, Sauda Simba na Witness The Fitness) tuko confused. Hatujui pakugeukia. Madansa wamepamba moto kinoma. Lakini hatimae ilibidi kapo moja waage shindano la TIKISA. Michael  Kayebo, japo ni mkali, gemu na patna wake Joyce Beatus halikua juu yakutosha kubaki katika shindano hili. Lakini mimi ninaamini hawa wawili watafika mbali kati fani ya dansi. Huu ni mwanzo tu. Niliwahamasisha wasikate tamaa.

TIKISA WIKI HII
Ogopa! Manake wiki iliyopita haioni ndani hata kwa dawa. Kuna watemi na wababe humu ndani sasa hivi, chungu kimechamka. Wamenichanganya. Pakugeukia sioni. Hali imekua ya joto kali. Jasho lanitoka. Pressure imepanda. Ilibidi niwaambie crew wapandishe viyoyozi manake kupumua ilikua taabu tupu. BIG UP kwa hawa wana TIKISA kwa kuleta burudani safi ITV. Kipindi tume shoot jana. Kesho, Jumamosi saa nne usiku, kitarushwa ITV. Mambo yameiva. Msikose!

Joett
Vocal Coach | Singer | Dancer Choreographer
Listen to Joett's New Single on Jango Internet Radio
Follow Joett On Twitter
Joett on Facebook
Email: info[at]joettmusic[dot]com 
 

No comments:

Post a Comment