Thursday, April 30, 2020

#Vokoz Online: Jifunze Kuimba na Joett kwa Njia ya Simu


VOKOZ, UTANGULIZI

Kwa wale ambao hawakufanikiwa kuingia kwenye program ya Vokoz ya Lady Jaydee na Joett, msife moyo. Kwani kuna uwezekano pia, wakujifunza kupitia program ambazo tayari nimeshaziandaa online, ni kiasi cha wewe ku-download MP3 na Makala zangu tu. (Tafadhali bofya hyperlinked text ili kufungua blog post husika).


Sauti ya Japhy Ross Kabla na 
Baada ya Mazoezi ya Sauti kwa Joett


Kabla ya Mazoezi ya Sauti


Baada ya Masaa 10 ya Mazoezi ya Sauti


Baada ya Miezi 10 ya Mazoezi ya Sauti


Jifunze Kuimba na Joett kwa Njia ya Simu

Huu ni utaratibu wa kujifunza kwa njia ya simu kwa kutumia voice/video call WhatsApp na Skype. Tafadhali fuata maelekezo yafuatayo.

STEP 1

Imba alafu unitumia sauti nikupe tathmini.

STEP 2

Feedback: nitakupa kuhusu sauti yako

STEP 3

Jinsi ambavo naweza kukusaidia, chukua madarasa 4 ya Dakika 30 kila darasa, kwa njia ya simu (voice/video call) WhatsApp au Skype (Skype ID yangu: tojona).

Bei kwa darasa moja la dakika 30 ni TZS 21,000.

BONUS PACKAGE

Ukinunua Madarasa Manne kwa Mpigo utapata madarasa ya dakika 45 badala ya dakika 30. Ambayo ni sawa sawa na jumla ya dakika 60 za ziada.

Utakapo kua tayari kuanza madarasa malipo utafanya kwa Admin wangu Hance Mligo kupitia M-Pesa +255 768 274 654 na kama wewe upo nje ya Africa Mashariki unaweza kutumia WorldRemit.

Maandalizi Maalum

VOICE/VIDEO CALL

Tunatumia voice/video call.

SPIKA (External Speakers)

Hakikisha simu yako imeunganishwa na spika (external speakers) kama speaker ya bluetooth au home theater, ili uweze kusikia sauti ya kinanda kama ilivyo.

VIFAA NYONGEZA

Ukiwa na device nyingine moja, yaani smartphone, tablet au computer, nitaweza kukurushia mazoezi ambayo ntatengeneza na kurusha ili uweze ku-play kwenye speaker huku tupo kwenye simu nikisikiliza ukifanya mazoezi.

MAZOEZI NDANI YA CHUMBA 

Hakikisha unafanya mazoezi haya ndani ya chumba. Sio nje.

Nahitaji information zako, yaani Jina Kamili, Umri, Namba ya Simu, anuani yako ya Barua Pepe. Hii chart nitaijaza mimi kwa kalamu hapa studio na itakua ndio faili yako.

Vocal Coaching                                                 Sessions Log

Name_______________________      Age______             Mobile #

Email_______________________

Date
Start Time
Vocal Exercise
Session Duration
Signature





















































TAHADHARI: COVID-19 

Ningependa pia kuwataarifuni ya kwamba kwa kipindi hiki cha kusambaa kwa ugonjwa wa Corona, madarasa yote nitakua nafanya kwa njia ya simu mpaka hapo hali itakapo badilika. Kizuri ni kwamba ninao uzoefu mkubwa wa kufundisha kwa njia ya simu.

Joett Voice Studio WhatsApp Group (BURE)

STEP 1 - Tuma vocal kwa voice note nikupe tathmini. WhatsApp +255 787 364 045

STEP 2 - Ntakupa zoezi fupi la sauti ufanye, jirekodi nitumie.

STEP 3 - Download mazoezi kutoka Mkito 

STEP 4 - Angalia video (bofya hapa) ya mifano ya hayo mazoezi (Vol. 1-4) na njia tofauti za kuyafanya ili kuimarisha sauti; na usome makala yangu (bofya hapa).
STEP 5 - Join link ya WhatsApp group (bofya hapa). 

STEP 6 - Jiandae kufanya darasa fupi (BURE) la uhakiki wa mazoezi kwa njia ya simu. Dakika 10 tu. (Maekelezo utapata baadae ndani ya group).


Karibuni,



Joett – Mwalimu wa Sauti



Saturday, April 11, 2020

Mazoezi ya Sauti, na Jinsi ya Kujipatia Msingi Mzuri na Mwalimu


Kujifunza kuimba kwa kutumia program zangu nilizopandisha Mkito; au kwa kutumia program ninazo stream Tumblr; au ninazorusha kwenye WhatsApp group zangu Joett Voice Studio na Gonga Jiwe for Joett, ni njia moja wapo ya kujifunza kuimba nyumbani kwako, mradi ufuate mungozo wangu na ushauri ninaoutowa kwenye makala zangu, na pia kwa kuzingatia mifano ya video nilizopandisha Facebook; na pia kuna video yenye mifano ya Joett Vocal Drills Vol. 1-4 (bofya hapa).

Kuna watu wanaonifuata Inbox na kuniambia kwamba wanashindwa kujifunzia nyumbani. Hii hali nnaielewa sana, lakini kama unataka kujifunza bila ya gharama yoyote, basi hauna budi kujitahidi pole pole hadi uweze kufanikiwa.

Sitaki kumdanganya mtu. Kuna watu ambao nimekutana nao ndani ya studio yangu baada ya wao kujaribu mazoezi yangu nyumbani kwa muda mrefu... miezi, hata mwaka na zaidi, ambao nilipowasikiliza walikua ni kama watu hawajawahi kufanya mazoezi ya sauti hata siku moja.

Na nilipo kaa nao kufanya tathmini tu ya sauti zao (huduma ya bure), niliweza kuwaweka sawa haraka sana, ndani ya muda wa dakika 30 tu, ambapo walikua wamepambana nyumbani kimakosa kwa muda mrefu bila ya mafanikio.

Watu hutofautiana katika kujifunza. Hata wale ambao nimekutana nao katika mazingira hayo hayo na walikua wamepiga hatua kubwa, wao pia kwa darasani mwangu niliweza kuwapeleka mbali zaidi.

Sababu ya mimi kutoa mazoezi ya sauti kwa njia ya mtandao lengo langu ni kuwasaidia waTanzania wenzangu kupata angalau uelewa, na mazoezi stahiki ili waweze kujiendeleza bila swala la gharama kua ndio kikwazo kwao.

Hivyo basi, mazoezi ya ana kwa ana ya kulipia yapo, japo ni watu wachache sana ambao wapo tayari kulipia mafunzo ya aina hii... hususan madarasa ya kujifunza muziki, iwe: sauti, guitar, kinanda na kadhalika.

Hii ndio hali halisi ilivo kwa hapa Tanzania.

Kwa sisi waalimu, ni kazi ambayo bila ya kujitolea tu kuwasaidia wanaotaka kuendeleza vipaji vyao, hii elimu itakua ni ngumu sana kuifikisha kwa walengwa.

Ningependa kurudia tena, kama kuna mtu yoyote ambae ana hisi angependa kupata msingi mzuri kwa kupitia madarasa ya kulipia, basi ni vyema awasiliane na mimi kwa njia ya simu au WhatsApp.

Kwa wale ambao mpo ndani ya WhatsApp groups Joett Voice Studio na Gonga Jiwe for Joett, jaribu kuwasiliana na Admin wangu wa hizo group, Hance Mligo, (bofya hapa) ili kupata utaratibu wa madarasa kwa njia ya simu (voice call) kupitia WhatsApp na Skype.


Wewe ndie chombo halisi, jifunze kuimba kama pro! 


JOETT - Mwalimu wa Sauti 




Thursday, April 9, 2020

Lady Jaydee na Joett Wanakuletea "Vokoz" Kuelimisha Waimbaji


PRESS RELEASE -- Kipindi kipya cha Vokoz kimeanzishwa na Lady Jaydee na Joett kwa madhumuni ya kuwasaidia vijana na wasanii chipukizi wa Tanzania na East Africa kufikia malengo yao katika swala zima la kujifunza uimbaji bora.

Mlolongo wa hili zoezi uko kama ifuatavyo.

Mwalimu wa sauti Joett anatoa tathmini ya sauti ana kwa ana, kwa wote ambao wamechaguliwa kuonana nae baada ya kutuma kwa Lady Jaydee kupitia DM ya akaunt yake Instagram, historia yao fupi ya kimuziki pamoja na sauti wakiimba.

Baada ya tathmini ya sauti, Lady Jaydee na Joett watakaa kikao kuamua nani wamuendeleze kwenye mafunzo hayo ya sauti ya ana kwa ana.

Baada ya mafunzo kwa kipindi cha takriban madarasa 10, Lady Jaydee atakaa na baadhi ya hawa wanafunzi ili kuwasaidia katika utunzi wa mashairi na kurekodi nyimbo studio.

Baada ya kurekodi nyimbo Lady Jaydee atachagua nani ampe nafasi ya kufanya show na yeye kwenye jukwa lake maalum la 20th Anniversary ya Lady Jaydee.

Unaweza kuangalia Vokoz Episode 1, 2, 3 & 4 hapa chini. Kumbuka ku-Subscribe YouTube Channel ya Lady Jaydee ili uweze kufuatilia vipindi vijavyo.







Subscribe YouTube channel ya Lady Jaydee, bofya hapa!

Ushuhuda wa Faida ya Mafunzo ya Sauti

Kwenye swala hili zima la uimbaji natumaini mngependa kufahamu, je sauti inaweza kufunguka au kubadilika kwa kiwango gani?

Sasa basi, ili kuwapa uelewa zaidi kuhusu faida ya mafunzo ya sauti kwa muimbaji, angalia video zifuatazo za mwanafunzi wa Joett ajulikanae kwa jina la kisanii kama Japhy Ross.

Japhy Ross, mkazi wa Mwanza, kabla ya mazoezi ya sauti alirekodi wimbo "Angejua" jijini Mwanza. Sikiliza video clip fupi ifuatayo.



Baada ya masaa 10 darasani na Joett, Japhy Ross alirekodi upya wimbo "Angejua" pale Wanene Studio, Dar es salaam. Sikiliza video clip fupi ifuatayo.


Baada ya miezi 10 darasani na Joett, Japhy Ross alirejea Mwanza
 na kurekodi wimbo mpya "Unanifaa". 
Sikiliza video clip fupi ifuatayo.


MAZOEZI YA SAUTI KWA WOTE

Kwavile nafasi ni chache katika zoezi hili la Vokoz, na kwavile madhumuni ya zoezi hili ni kutoa elimu kwa wote, tungependa kukaribisha wote ambao wangependa kuboresha uimbaji wao, wajiunge na huduma ya Joett ambayo inatolewa  bila gharama kupitia mtandao.

Yaani hapa utakutana na group lake la WhatsApp na pia utaweza ku-download mazoezi ambayo amepandisha Mkito pamoja na ku-stream mazoezi aliyopandisha Tumblr.

Ili kupata maelezo zaidi tafadhali soma makala yake: "Unahitaji Mazoezi ya Sauti? Download Joett Vocal Drills Vol. 1-7!"

Natumaini kwa namna moja au nyingine mmenufaika na yaliyomo kwenye hii blog post. Tunawaomba mjisikie huru ku-share.


Wewe ndie chombo halisi, jifunze kuimba kama pro! 



JOETT - Mwalimu wa Sauti

Makala Zifuatazo ni Muhimu Kusoma (bofya links)

Unahitaji Mazoezi ya Sauti? Download Joett Vocal Drills Vol. 1-7!
Msaada wa Mafunzo ya Sauti na JOETT WhatsApp na Telegram
Je, Binadamu Anaimbia Tumboni? Jua Ule Ukweli Wenyewe Halisi
Jifunze Kuimba na Joett Darasani na Online: Muongozo na Utaratibu
Jifunze Kuimba: Umuhimu wa Kuelewa Madhumuni Ya Mazoezi
Jifunze Kuimba: Tatizo La Pumzi na Jinsi Ya Kulitatua
Kujifunza Kuimba Kwa Kupiga Makelele Hakusaidii Lolote
Jifunze Kuimba na Joett Mkito.com Vol. 1: Madhumuni ya Lip Rolls
Je, Utajuaje Kama Unakosea Katika Mazoezi Ya Sauti ?
Jiunge na Darasa Moja La Kukusaidia Ukae Sawa na Mazoezi Ya Sauti


Monday, March 23, 2020

Corona Pandemic Self-Isolation: Virtual Singing Lessons Worldwide

If you are cooped up at home in self-isolation due to the corona virus outbreak around the world and you’re running out of ideas for keeping yourself occupied, then you will find that you can perhaps spend a bit of that spare time learning to sing with an online voice coach on Skype.

This article will aim to open up an idea for an extracurricular activity you may want to consider for keeping yourself occupied AND entertained during the dreaded COVID19 pandemic that has spread across the planet and brought about an all new social distancing phenomenon.

So, assuming you want to learn to sing, and given the current situation with economies around the globe, the first thing you’ll want to consider is the cost associated with hiring a voice coach.

How much is this going to cost? 

It's far less than you'd expect.

To get an idea of the quality of service to be expected on this platform and the incredibly affordable rate this service is offered to you, please check out the embedded video clip below.


I’ve written a couple of articles on this topic before. This is how you can get stuck right in to find out a bit more about my Personalized Vocal Coaching on Skype for Europe and North America; and you can also pick-up information on How to Set-up for Voice Lessons with a Coach on Skype.


If you’ve been wondering what else to do to keep yourself occupied and entertained during the corona virus outbreak, my hyperlinked articles placed in this blog post will talk you through getting started with voice lessons with a professional vocal coach on Skype. Now the following is how to book your online voice lessons with JOETT.



BOOK YOUR PLACE TODAY

We accept payment by Credit, Debit Cards and PayPal via the Nam Radio platform, and we’ll discuss the details of the training programs when you get in touch with me.


You are the Instrument, Learn to Sing Like a pro!



JOETT – Voice Coach & Author:
101 Letters from a Vocal Coach


Friday, March 6, 2020

Diary of a Voice Coach, a Quick Reflection on Previous Articles

unsplash-logoNick Morrison
I haven’t blogged in a while and I myself cannot believe it’s been this long, crazy how time flies.

I suppose I needed the break too. I must’ve gotten tired writing, I’ve been doing this for so many years.

I remember the time when I had a weekly newspaper column and deadlines to meet. Well, the good thing about that is I was finally able to write enough content to publish my book 101 Letters from a Vocal Coach.

Back in October last year I blogged about a crowd-funding event I’d started up on Fundly. There’s been no activity whatsoever and I haven’t raised a dime thus far. Maybe I need to get stuck back in with promoting that. Who knows what’ll come out of this, but it would be nice if people joined me to promote the link. It is the only way I can raise funds to help others. I cannot do it on my own. I simply don’t have the resources.

Voice coaching online via Skype is something I’ve been putting in a bit of time with of late, and I’ve been gradually refining the service. I like the look of it now, far better. Just a couple of days ago I updated my Skype blog post, where you’ll find that I’ve added a bit more detail on how best to set-up for voice lessons via Skype.

My 12-minute vocal warm-up, which links back to Tumblr where I have embedded mp3, has had a few more files added to it for the Swahili speaking crowd. I might republish this content in English.

I hope you've enjoyed my first article of 2020. Stay well and talk to you soon.

You are the Instrument, Learn to Sing Like a Pro!


JOETT - Vocal Coach & Author:
101 Letters from a Vocal Coach

Sunday, December 1, 2019

The Simplest Ever, Steps to Placing Your Tone in the Mask

If you’ve been reading my articles or perhaps you’ve read my book, you will by now be familiar with what singing in the mask is all about.

This short article will offer tips on why a resonant voice is so important for singers, and it begins with the art of placing your tone in the mask in voice training so that it resonates; extends your vocal range; and adds timbre and color to your tone.

And you’re going to be surprised to discover just how easy it is to develop a beautifully unique tonee, because already, you ARE unique—well, everybody’s voice is unique because our skulls are all unique… even in the case of identical twins, there is always a slight difference in the shape and size of the skull.

Why is the skull significant? 

Because the voice resonates in the head and this is what creates a sound that is especially unique to every individual on the planet. To properly harness and develop this unique sound as a singer, the way to go about it is to master Speech Level Singing Technique.

There’s nothing complicated about this. It is just a combination of vocal exercises that will help to connect your bottom, middle and upper harmonic qualities in order to develop one strong and dynamic voice. I think that is the simplest way of putting this.

Special Vocal Exercises

Included with my book, you’ll find my vocal exercises Joett Vocal Drills Volumes 1-7. Better yet, I’d be more than happy to give you a FREE voice assessment via WhatsApp. (You’ll find my WhatsApp number in the banner above).

In the meantime, if you’d like to get started FREE straight away, stream some of my vocal exercises included in my article How to Get a Complete Vocal Warm-Up in Just 12 Minutes.

If you like this article, please be so kind as to share on your social media using the links below. And you can book private voice lessons with me here!

You are the Instrument, Learn to Sing Like a Pro!


JOETT - Voice Coach & Author
101 Letters from a Vocal Coach



Unahitaji Mazoezi ya Sauti? Download Joett Vocal Drills Vol. 1-7!


Kwanza kabisa, tafadhali imba, jirekodi, alafu nitumie voice note WhatsApp ili niweze kufanya tathmini ya sauti na uimbaji wako. Baada ya hapo, soma yafuatayo kwenye hii makala na uhakikishe unabofya link zilizomo humu ndani kwa maelezo husika ya ziada.

Sinabudi kuwajulisha yakwamba makala zangu zina mafunzo ya kina kuhusu uimbaji bora. Muhimu kusoma ili usipitwe na mambo muhimu.

Kama ungependa ku-download mazoezi yangu ya sauti (Joett Vocal Drills Vol 1-7) na imekushinda kupitia Mkito, basi kupitia blog langu la Tumblr unaweza ku-stream Zoezi la Pumzi na Joett Vocal Drills Vol. 1, Joett Vocal Drills Vol. 2, Joett Vocal Drills Vol. 3, Joett Vocal Drills Vol. 4.

Mifano ya Joett Vocal Drills Vol. 1-4

Nimetengeneza video darasani kwangu (bofya hapa) ili kuwaonyesha jinsi ya kufanya mazoezi yangu ya Joett Vocal Drills Vol. 1-4, pamoja na njia zingine za kutumia scales hizo hizo kufanya mazoezi tofauti (yaani alternative vocal excercises).

Usifanye zoezi kwa njia nyingine tofauti na nilivoonyesha hapa. Tafadhali tazama video (bofya hapa) na ufuatilie mifano hii kwa umakini sana. Utagundua kwamba haitumiki nguvu kufanya haya mazoezi.

  1. Kwa maelekezo zaidi kuhusu mazoezi ya sauti bofya hapa!
  2. Kwa ratiba ya mazoezi bofya hapa!
  3. Kwa mazoezi ya ziada bofya hapa!
  4. Uimbaji Bora: Maswali na Majibu bofya hapa!
  5. Kujiunga na Group la WhatsApp bofya hapa! 
  6. Kujiunga na Group la Facebook bofya hapa!
  7. Kwa madarasa ya ana kwa ana bofya hapa!
  8. Kwa maelekezo ya ku-login Mkito kwa kutumia akaunti yako ya Google angalia video hapa chini!


    JUMP START PROGRAM
(Dakika 30 Tu kwa Njia ya Simu)

Mazoezi ya Sauti na Joett kwa njia ya simu ya WhatsApp na Skype kwa Dakika 30 tu ni ratiba mpya ambayo hutolewa kwa njia ya simu (voice call) kupitia app za WhatsApp na Skype. Skype ni bora zaidi kwa hili zoezi, itakua vyema uki-download app kutoka Play Store au App Store.

"Zingatia Haya Maandalizi Maalum"

VOICE CALL

Tunatumia voice call. Sio video call.

SPIKA (External Speakers)

Hakikisha simu yako imeunganishwa na spika (external speakers) kama speaker ya bluetooth au home theater, ili uweze kusikia sauti ya kinanda kama ilivyo.

MAZOEZI NDANI YA CHUMBA 

Hakikisha unafanya mazoezi haya ndani ya chumba. Sio nje.

Joett Voice Studio WhatsApp Group

Kufanya booking ya madarasa haya ya njia ya simu, tafadhali bofya hapa!


WhatsApp Group zipo mbili: Joett Voice Studio na Gonga Jiwe for Joett.

================================

Huduma ya Ziada (Bure)

Ukihitaji kuhakiki kama unayafanya mazoezi kifasaha, jirekodi ukifanya haya mazoezi alafu tuma mazoezi yako kwangu kwa njia ya WhatsApp. Mifano ya mazoezi haya utayakuta kwenye Facebook page yangu hapa!

Video zifuatazo ni safari ya Japhy Ross katika kujifunza kuimba na JOETT


Uimbaji wa Japhy Ross kabla ya Mazoezi ya Sauti 


Uimbaji wa Japhy Ross Baada ya Masaa 10 ya Mazoezi 



Uimbaji wa Japhy Ross baada ya Miezi 10 ya Mazoezi 


Makala Zifuatazo ni Muhimu Kusoma (bofya links)

Msaada wa Mafunzo ya Sauti na JOETT WhatsApp na Telegram
Je, Binadamu Anaimbia Tumboni? Jua Ule Ukweli Wenyewe Halisi
Jifunze Kuimba na Joett Darasani na Online: Muongozo na Utaratibu
Jifunze Kuimba: Umuhimu wa Kuelewa Madhumuni Ya Mazoezi
Jifunze Kuimba: Tatizo La Pumzi na Jinsi Ya Kulitatua
Kujifunza Kuimba Kwa Kupiga Makelele Hakusaidii Lolote
Jifunze Kuimba na Joett Mkito.com Vol. 1: Madhumuni ya Lip Rolls
Je, Utajuaje Kama Unakosea Katika Mazoezi Ya Sauti ?
Jiunge na Darasa Moja La Kukusaidia Ukae Sawa na Mazoezi Ya Sauti

Nawatakia mafanikio mema!



JOETT - Mwalimu wa Sauti