Thursday, April 30, 2020

#Vokoz Online: Jifunze Kuimba na Joett kwa Njia ya Simu


VOKOZ, UTANGULIZI

Kwa wale ambao hawakufanikiwa kuingia kwenye program ya Vokoz ya Lady Jaydee na Joett, msife moyo. Kwani kuna uwezekano pia, wakujifunza kupitia program ambazo tayari nimeshaziandaa online, ni kiasi cha wewe ku-download MP3 na Makala zangu tu. (Tafadhali bofya hyperlinked text ili kufungua blog post husika).


Sauti ya Japhy Ross Kabla na 
Baada ya Mazoezi ya Sauti kwa Joett


Kabla ya Mazoezi ya Sauti


Baada ya Masaa 10 ya Mazoezi ya Sauti


Baada ya Miezi 10 ya Mazoezi ya Sauti


Jifunze Kuimba na Joett kwa Njia ya Simu

Huu ni utaratibu wa kujifunza kwa njia ya simu kwa kutumia voice/video call WhatsApp na Skype. Tafadhali fuata maelekezo yafuatayo.

STEP 1

Imba alafu unitumia sauti nikupe tathmini.

STEP 2

Feedback: nitakupa kuhusu sauti yako

STEP 3

Jinsi ambavo naweza kukusaidia, chukua madarasa 4 ya Dakika 30 kila darasa, kwa njia ya simu (voice/video call) WhatsApp au Skype (Skype ID yangu: tojona).

Bei kwa darasa moja la dakika 30 ni TZS 21,000.

BONUS PACKAGE

Ukinunua Madarasa Manne kwa Mpigo utapata madarasa ya dakika 45 badala ya dakika 30. Ambayo ni sawa sawa na jumla ya dakika 60 za ziada.

Utakapo kua tayari kuanza madarasa malipo utafanya kwa Admin wangu Hance Mligo kupitia M-Pesa +255 768 274 654 na kama wewe upo nje ya Africa Mashariki unaweza kutumia WorldRemit.

Maandalizi Maalum

VOICE/VIDEO CALL

Tunatumia voice/video call.

SPIKA (External Speakers)

Hakikisha simu yako imeunganishwa na spika (external speakers) kama speaker ya bluetooth au home theater, ili uweze kusikia sauti ya kinanda kama ilivyo.

VIFAA NYONGEZA

Ukiwa na device nyingine moja, yaani smartphone, tablet au computer, nitaweza kukurushia mazoezi ambayo ntatengeneza na kurusha ili uweze ku-play kwenye speaker huku tupo kwenye simu nikisikiliza ukifanya mazoezi.

MAZOEZI NDANI YA CHUMBA 

Hakikisha unafanya mazoezi haya ndani ya chumba. Sio nje.

Nahitaji information zako, yaani Jina Kamili, Umri, Namba ya Simu, anuani yako ya Barua Pepe. Hii chart nitaijaza mimi kwa kalamu hapa studio na itakua ndio faili yako.

Vocal Coaching                                                 Sessions Log

Name_______________________      Age______             Mobile #

Email_______________________

Date
Start Time
Vocal Exercise
Session Duration
Signature





















































TAHADHARI: COVID-19 

Ningependa pia kuwataarifuni ya kwamba kwa kipindi hiki cha kusambaa kwa ugonjwa wa Corona, madarasa yote nitakua nafanya kwa njia ya simu mpaka hapo hali itakapo badilika. Kizuri ni kwamba ninao uzoefu mkubwa wa kufundisha kwa njia ya simu.

Joett Voice Studio WhatsApp Group (BURE)

STEP 1 - Tuma vocal kwa voice note nikupe tathmini. WhatsApp +255 787 364 045

STEP 2 - Ntakupa zoezi fupi la sauti ufanye, jirekodi nitumie.

STEP 3 - Download mazoezi kutoka Mkito 

STEP 4 - Angalia video (bofya hapa) ya mifano ya hayo mazoezi (Vol. 1-4) na njia tofauti za kuyafanya ili kuimarisha sauti; na usome makala yangu (bofya hapa).
STEP 5 - Join link ya WhatsApp group (bofya hapa). 

STEP 6 - Jiandae kufanya darasa fupi (BURE) la uhakiki wa mazoezi kwa njia ya simu. Dakika 10 tu. (Maekelezo utapata baadae ndani ya group).


Karibuni,



Joett Mwalimu wa Sauti



Saturday, April 11, 2020

Mazoezi ya Sauti, na Jinsi ya Kujipatia Msingi Mzuri na Mwalimu


Kujifunza kuimba kwa kutumia program zangu nilizopandisha Mkito; au kwa kutumia program ninazo stream Tumblr; au ninazorusha kwenye WhatsApp group zangu Joett Voice Studio na Gonga Jiwe for Joett, ni njia moja wapo ya kujifunza kuimba nyumbani kwako, mradi ufuate mungozo wangu na ushauri ninaoutowa kwenye makala zangu, na pia kwa kuzingatia mifano ya video nilizopandisha Facebook; na pia kuna video yenye mifano ya Joett Vocal Drills Vol. 1-4 (bofya hapa).

Kuna watu wanaonifuata Inbox na kuniambia kwamba wanashindwa kujifunzia nyumbani. Hii hali nnaielewa sana, lakini kama unataka kujifunza bila ya gharama yoyote, basi hauna budi kujitahidi pole pole hadi uweze kufanikiwa.

Sitaki kumdanganya mtu. Kuna watu ambao nimekutana nao ndani ya studio yangu baada ya wao kujaribu mazoezi yangu nyumbani kwa muda mrefu... miezi, hata mwaka na zaidi, ambao nilipowasikiliza walikua ni kama watu hawajawahi kufanya mazoezi ya sauti hata siku moja.

Na nilipo kaa nao kufanya tathmini tu ya sauti zao (huduma ya bure), niliweza kuwaweka sawa haraka sana, ndani ya muda wa dakika 30 tu, ambapo walikua wamepambana nyumbani kimakosa kwa muda mrefu bila ya mafanikio.

Watu hutofautiana katika kujifunza. Hata wale ambao nimekutana nao katika mazingira hayo hayo na walikua wamepiga hatua kubwa, wao pia kwa darasani mwangu niliweza kuwapeleka mbali zaidi.

Sababu ya mimi kutoa mazoezi ya sauti kwa njia ya mtandao lengo langu ni kuwasaidia waTanzania wenzangu kupata angalau uelewa, na mazoezi stahiki ili waweze kujiendeleza bila swala la gharama kua ndio kikwazo kwao.

Hivyo basi, mazoezi ya ana kwa ana ya kulipia yapo, japo ni watu wachache sana ambao wapo tayari kulipia mafunzo ya aina hii... hususan madarasa ya kujifunza muziki, iwe: sauti, guitar, kinanda na kadhalika.

Hii ndio hali halisi ilivo kwa hapa Tanzania.

Kwa sisi waalimu, ni kazi ambayo bila ya kujitolea tu kuwasaidia wanaotaka kuendeleza vipaji vyao, hii elimu itakua ni ngumu sana kuifikisha kwa walengwa.

Ningependa kurudia tena, kama kuna mtu yoyote ambae ana hisi angependa kupata msingi mzuri kwa kupitia madarasa ya kulipia, basi ni vyema awasiliane na mimi kwa njia ya simu au WhatsApp.

Kwa wale ambao mpo ndani ya WhatsApp groups Joett Voice Studio na Gonga Jiwe for Joett, jaribu kuwasiliana na Admin wangu wa hizo group, Hance Mligo, (bofya hapa) ili kupata utaratibu wa madarasa kwa njia ya simu (voice call) kupitia WhatsApp na Skype.


Wewe ndie chombo halisi, jifunze kuimba kama pro! 


JOETT - Mwalimu wa Sauti 




Thursday, April 9, 2020

Lady Jaydee na Joett Wanakuletea "Vokoz" Kuelimisha Waimbaji


PRESS RELEASE -- Kipindi kipya cha Vokoz kimeanzishwa na Lady Jaydee na Joett kwa madhumuni ya kuwasaidia vijana na wasanii chipukizi wa Tanzania na East Africa kufikia malengo yao katika swala zima la kujifunza uimbaji bora.

Mlolongo wa hili zoezi uko kama ifuatavyo.

Mwalimu wa sauti Joett anatoa tathmini ya sauti ana kwa ana, kwa wote ambao wamechaguliwa kuonana nae baada ya kutuma kwa Lady Jaydee kupitia DM ya akaunt yake Instagram, historia yao fupi ya kimuziki pamoja na sauti wakiimba.

Baada ya tathmini ya sauti, Lady Jaydee na Joett watakaa kikao kuamua nani wamuendeleze kwenye mafunzo hayo ya sauti ya ana kwa ana.

Baada ya mafunzo kwa kipindi cha takriban madarasa 10, Lady Jaydee atakaa na baadhi ya hawa wanafunzi ili kuwasaidia katika utunzi wa mashairi na kurekodi nyimbo studio.

Baada ya kurekodi nyimbo Lady Jaydee atachagua nani ampe nafasi ya kufanya show na yeye kwenye jukwa lake maalum la 20th Anniversary ya Lady Jaydee.

Unaweza kuangalia Vokoz Episode 1, 2, 3 & 4 hapa chini. Kumbuka ku-Subscribe YouTube Channel ya Lady Jaydee ili uweze kufuatilia vipindi vijavyo.







Subscribe YouTube channel ya Lady Jaydee, bofya hapa!

Ushuhuda wa Faida ya Mafunzo ya Sauti

Kwenye swala hili zima la uimbaji natumaini mngependa kufahamu, je sauti inaweza kufunguka au kubadilika kwa kiwango gani?

Sasa basi, ili kuwapa uelewa zaidi kuhusu faida ya mafunzo ya sauti kwa muimbaji, angalia video zifuatazo za mwanafunzi wa Joett ajulikanae kwa jina la kisanii kama Japhy Ross.

Japhy Ross, mkazi wa Mwanza, kabla ya mazoezi ya sauti alirekodi wimbo "Angejua" jijini Mwanza. Sikiliza video clip fupi ifuatayo.



Baada ya masaa 10 darasani na Joett, Japhy Ross alirekodi upya wimbo "Angejua" pale Wanene Studio, Dar es salaam. Sikiliza video clip fupi ifuatayo.


Baada ya miezi 10 darasani na Joett, Japhy Ross alirejea Mwanza
 na kurekodi wimbo mpya "Unanifaa". 
Sikiliza video clip fupi ifuatayo.


MAZOEZI YA SAUTI KWA WOTE

Kwavile nafasi ni chache katika zoezi hili la Vokoz, na kwavile madhumuni ya zoezi hili ni kutoa elimu kwa wote, tungependa kukaribisha wote ambao wangependa kuboresha uimbaji wao, wajiunge na huduma ya Joett ambayo inatolewa  bila gharama kupitia mtandao.

Yaani hapa utakutana na group lake la WhatsApp na pia utaweza ku-download mazoezi ambayo amepandisha Mkito pamoja na ku-stream mazoezi aliyopandisha Tumblr.

Ili kupata maelezo zaidi tafadhali soma makala yake: "Unahitaji Mazoezi ya Sauti? Download Joett Vocal Drills Vol. 1-7!"

Natumaini kwa namna moja au nyingine mmenufaika na yaliyomo kwenye hii blog post. Tunawaomba mjisikie huru ku-share.


Wewe ndie chombo halisi, jifunze kuimba kama pro! 



JOETT - Mwalimu wa Sauti

Makala Zifuatazo ni Muhimu Kusoma (bofya links)

Unahitaji Mazoezi ya Sauti? Download Joett Vocal Drills Vol. 1-7!
Msaada wa Mafunzo ya Sauti na JOETT WhatsApp na Telegram
Je, Binadamu Anaimbia Tumboni? Jua Ule Ukweli Wenyewe Halisi
Jifunze Kuimba na Joett Darasani na Online: Muongozo na Utaratibu
Jifunze Kuimba: Umuhimu wa Kuelewa Madhumuni Ya Mazoezi
Jifunze Kuimba: Tatizo La Pumzi na Jinsi Ya Kulitatua
Kujifunza Kuimba Kwa Kupiga Makelele Hakusaidii Lolote
Jifunze Kuimba na Joett Mkito.com Vol. 1: Madhumuni ya Lip Rolls
Je, Utajuaje Kama Unakosea Katika Mazoezi Ya Sauti ?
Jiunge na Darasa Moja La Kukusaidia Ukae Sawa na Mazoezi Ya Sauti