Wednesday, December 8, 2010

Joett Arejea No Single Mpya

PRESS RELEASE YA REDIO -- Mwalimu wa kuimba wa kitanzania, Joett, ambae single yake ya kwanza iitwayo “Afro Lover” ili fika namba sita kwenye chati za dansi inchini Uingereza mwaka 1996, na kupigwa kwenye vilabu na hadi kutolewa kwenye compilation album kadhaa za dansi Uingereza, Ulaya na Arabuni, amerudi na kibao kipya kiitwacho “I Could Never Live (Without Your Love)” – tafsiri yake ikiwa… “Siwezi Kuishi (Bila Penzi Lako)”. Rekodi hiyo mpya inaingia sokoni ulimwenguni tarehe 20 Desemba 2010 kupitia Island Def Jam Digital Distribution iliopo inchini Marekani. Kibao hicho kipya kilirekodiwa sauti ya msanii huyo pamoja na acoustic guitar (ikipigwa na Ashimba), pale 41 Records, Dar es salaam, na producer Ken Kanyeria; alafu, kwa kutumia kampuni ya kusafirishia vifurushi FEDEX, Joett alipeleka faili hizo za muziki katika studio ya kurekodia jijini London, Uingereza, kumalizia production, mixing, mastering na remixing ya kazi hiyo. Rekodi hiyo ina jumla ya track sita. Radio edit, remix, original acoustic version, na instrumental tatu. Joett, ambae ni mkazi wa jiji la Dar es salaam, ni mwalimu wa kuimba alie bobea katika fani hiyo, kutokana na mafunzo aliyoyapata nchini Uingereza. Anasema, “Ninafuraha sana kurejea katika fani ya kutengenza muziki, na hasa kufundisha watanzania wenzangu kuimba”.

Kwa Maelezo Zaidi Tembelea Blog yake: www.joettmusic.com
Au Piga Simu Namba: 0787 364 045 / 0715 364 045

No comments:

Post a Comment