Tuesday, December 6, 2016

Jifunze Kuimba na Joett Mkito.com: Vocal Drills Volume 2


Volume 2 ni muendelezo wa Vol. 1. Kwa maana ni lazima ufanye Vol. 1 kabla haujafanya Vol. 2. Kwa mara nyingine tena, nita sistiza mfuate maelekezo kama yalivo kwenye toleo hili. 

Mazoezi haya yana dakika 7. Ukishaweza kufanya haya mazoezi, sasa utakua na mazoezi mawili. Yaani Vol. 1 & 2 katika ratiba yako ya mazoezi ya sauti ya kila siku; na utatakiwa kufanya yote kwa pamoja kufuata mlolongo huo huo wa Vol. 1 kuingia Vol. 2.

Kumbuka, madhumuni ya haya mazoezi ni ku re-balance sauti yako, au kurekebisha matumizi ya sauti yako ili uweze kuimba kwa urahisi kwenda juu na kwenda chini; na mpangilio na ratiba hii ndio itaweza kukupa wewe huo uwezo kwa njia ya haraka na salama zaidi. Tafadhali usianze kukurupuka na ku-download vitu olela kwenye internet. Tafadhali fuata maelekezo yangu na mazoezi niliokuandalia ili uweze kupata mafanikio ya uhakika. Download Volume 2 hapa!

Na vile vile unaweza kupata maelekezo zaidi kwa kubofya nakala kadhaa nilizo andika hapa chini. Ukiwa na maswali, tafadhali jisikie huru kuniuliza. Ni muhimu sana kuelewa, na sio kufanya vitu kwa hisia bila muongozo panapo stahili. Tafuta ushauri!

Jifunze Kuimba: Umuhimu wa Kuelewa Madhumuni Ya Mazoezi
Jifunze Kuimba: Tatizo La Pumzi na Jinsi Ya Kulitatua
Jifunze Kuimba na Joett Mkito.com Vol. 1: Madhumuni ya Lip Rolls

Wewe ndie chombo halisi, jifunze kuimba kama pro!


JOETT
Vocal Coach
YouTube Channel

Friday, December 2, 2016

Jifunze Kuimba na Joett Darasani: Muongozo na Utaratibu Maalum

Ukitaka kujifunza kuimba ndani ya darasa langu studio, ana kwa ana, utaratibu ni kama ufuatavyo.

Kwanza kabisa, mimi ninafundisha siku 3 tu kwa wiki… Jumatatu, Jumanne na Jumatano, na ninachukua wanafunzi wachache sana kwa siku, kwasababu ninafundisha mtu mmoja mmoja tu kila lisaa kwa kufuata ratiba iliopangwa maalum. Kwahivyo nafasi za kuchukua wanafunzi wapya huaga ni adimu sana.

Program Zangu Za Mafunzo ya Sauti  ndani ya studio yangu katika mfumo wa Speech Level Singing Comprehensive Courses zipo kama ifuatavyo: Level 1, Level 2, Intermediate, Advanced, Pro, Pro 2 na Pro Club... na kila programu ni ya masaa 10. (Yaani, kila utakapokuja darasani utafanya mazoezi kaw lisaa limoja tu).

Quick Start Program 

Program ya Quick Start ni ya maandalizi na ni kwa ghrama bafuu, kukuwezesha wewe kwenda kufanya mazoezi mwenyewe nyumbani, na program hii ni ya masaa 3 tu ndani ya studio yangu.

1 Hour Vocal Training Session ni darasa la lisaa limoja tu kwa wale ambao wameshapitia msingi mzuri katika madarasa yangu ya ana kwa ana; na vile vile kwa wale wanaojifunza kupitia programu zangu za Jifunze Kuimba Na Joett Vocal Drills zinazopatikana Mkito.com. Darasa ilo limoja limoja linaweza kua kama nyongeza au "brush-up" ya mara kwa mara katika kujifunza kwako kuimba.

VOICE ASSESSMENTS (Ukaguzi wa Sauti)

Kabla haujaanza mafunzo ya ana kwa ana, nakukaribisha uje studio kwa dakika 30 tu niskie sauti yako, na vile vile nikupitishe kwenye mazoezi kadhaa kwenye kinanda ili niijue sauti yako na changamoto zako za kurekebisha.

Hua nafanya assessments—yaani ukaguzi wa sauti kwa wanafunzi wanaotaka kujiunga na madarasa yangu ya masaa 10—siku za Jumamosi kwa nusu saa bila gharama yeyote--ni bure, lakini kwa mihadi maalum ya muda wa assessment. Ili kupata nafasi ya assessment, tafadhali wasiliana na mimi kwa njia ya simu au kupitia WhatsApp.

DOWNLOAD TRAINING MKITO.COM

Jifunze kwa urahisi na kwa gharama nafuu ya Shs 250 tu, kwa ku-download program zangu nilizopandisha Mkito.com kwa ajili yako.

Kupitia mfumo huu, nimeboresha mazoezi maalum ya sauti kwa kufuata mahitaji muhimu katika kujifunza kuimba kupitia mtandao. Ili kuingia katika mstari stahiki wa mafunzo ambao bila shaka, utakuletea mafanikio ya haraka, ni vyema kuanza safari yako ya kujifunza kuimba hapa.

Na vile vile unaweza kupata maelekezo zaidi kwa kubofya nakala kadhaa nilizo andika hapa chini. Ukiwa na maswali, tafadhali jisikie huru kuniuliza. Ni muhimu sana kuelewa, na sio kufanya vitu kwa hisia bila muongozo panapo stahili. Tafuta ushauri!

Jifunze Kuimba: Umuhimu wa Kuelewa Madhumuni Ya Mazoezi

Wewe ndie chombo halisi, jifunze kuimba kama pro!


JOETT
Vocal Coach 


Monday, November 28, 2016

Discover The Incredible Vocal Range and Profile of Ariana Grande

This article will explore the incredible vocal range and profile of Ariana Grande. For your reading delight, I thought to publish a compilation of some rather interesting observations from critics of music, that highlight enlightening elements on the Vocal Range of Ariana Grande. I’m sure you will enjoy this!

With a light-lyric Soprano in the 4 octave range and a note, Ariana Grande’s vocal rating is said to be an A-List. Recommended listening in this regard therefore, are her songs Emotions and The Way. I think it is safe to consider Ariana as a vocal actress, being able to mimic the tones and voices of Britney Spears, Mariah Carey, Christina Aguilera and Celine Dion. Her lower register, however, is  often weak and inconsistent, due to—according to one critic—her high tessitura and breath support issues, yet she is relatively strong for a soprano, supporting down to F#3 and extending to D3.

She achieves her belts, as it were, through mixing, stretched up to Bb5's successfully. Grande also has no issue staying in the soprano tessitura for extended periods of time. If you watch her live performances of Break Free, Dangerous Woman and Focus you’ll get the picture. She has an extensive belting register as a whole and reaches up to an impressive B5, capable of complex, fast melismas as clearly evident in Hands on Me and Problem. She also has a rolling vibrato that can be heard in belts up to G#5 and as low as Bb3.

Her falsetto area is light and sweet, and is also where Ariana’s voice finds its ring, as it were, with a bright and healthy tone up to Eb6.

Ariana Grande’s whistle tone is undoubtedly piercing, and her whistles don't have disconnected tones attached to them. If you listen to her song Emotions, you’ll note that she is able to sing vocal runs in this register.

As you’d probably be well aware, there are no positives without the negatives. Of her own admission, her mixed belts generally lack power and the whistle register is not controlled. Her slightly nasal and feminine tone is also polarizing. Her diction, noted in 2013 as being unpolished, left her lyrics incomprehensible at points as you’ll see in the bridge of Break Free, and this is mainly due to tongue tension. Another thing about Grande, according to a music critic, is that she also over activates muscles in her jaw – mostly while singing runs – thereby furthering this tongue tension, which in turn changes the positioning of the larynx. That being said, again, according to a music critic, intonation live has proven to be a problem at points (around 2013), and the lower register sounded unsupported in most instances. Her support—it has been said, is also inconsistent, ranging from around G3-C#5. Above C#5 she raises her larynx.

I hope you enjoyed this interesting piece on Ariana Grande's AMAZING vocal range.


JOETT

Vocal Coach
"Letters from a Vocal Coach"

Saturday, November 26, 2016

Jifunze Kuimba na Joett Mkito.com Vol. 1: Madhumuni ya Lip Rolls

Kwenye mazoezi ya Joett Vocal Drills Vol. 1 utakutana na Lip Rolls na Tongue Trills. Zote nimeelekeza jinsi ya kufanya na kutoa mifano kwenye mp3 kabla ya kuanza mazoezi hayo.

Hapa ningependa tu kutoa maelekezo kuhusu malengo ya haya mazoezi mawili.

Kwa ufupi, yana ondoa tabia ya kuimbia kooni. Unapofanya haya mazoezi misuli ilioko nje ya koromelo lako haishtuki na kukaza. Hapo basi sauti inapata urahisi wakutembea kwenda juu na chini bila ya shiriksho hilo la misuli ya kooni katika utengenezaji wa sauti.

Ukizoea hili zoezi, baada ya muda, hii tabia ya utulivu wa misuli ya nje ya koromelo lako linakufuata katika kuimba nyimbo. Kama unashindwa kufanya Lip Rolls au Tongue Trills, jaribu kufanya mazoezi haya kwa kutamka “CCC au Sii” badala yake.

Muongozo wa Mazoezi

 • Download mazoezi Mkito.com
 • Weka kwenye CD au Flash Disk
 • Tumia chombo cha muziki cha kupigia CD/Flash au kama unatumia simu yako ya mkononi, hakikisha unaunganisha na speaker kupata sauti kubwa kulingana na sauti yako ukiimba. 
 • Fanya mazoezi ndani ya chumba na sio kwenye maeneo ya wazi, wala sio kwa kutumia simu yako ya mkononi na headset zake masikioni. 
 • Ku-Download PDF yenye maelekezo ya Volume 1, 2, 3 & 4 Bofya hapa!
 • Kusoma Press Release bofya hapa!

Ukiwa na maswali, jiskie huru kuniuliza, au soma nakala kadhaa nilizo andika:
Jifunze Kuimba: Umuhimu wa Kuelewa Madhumuni Ya Mazoezi
Jifunze Kuimba: Tatizo La Pumzi na Jinsi Ya Kulitatua

Wewe ndie chombo halisi, jifunze kuimba kama pro!


JOETT
Vocal Coach
Madarasa ya Studio

Understand the Importance of Focusing Your Tone

Singing is SO much fun. I’ve seen the joy that it brings to people. When their faces light up! Electrified and overwhelmed with joy when they’re hitting those notes nice and clean. It makes me feel like a miracle worker of sorts. Bringing so much joy to so many people couldn’t be more rewarding than this. What I want to talk about today is the importance of focusing your tone. You see, at the end of the day you’re going to be singing songs, and every word you project out of your mouth needs focus. So here’s your ‘quick tips’ article on how to maintain focus in tone production.

I love using the narrow vowels in training. They help focus the voice. Something like UIU is particularly good for narrowing down that focus to precisely what you want—focus. And a quick three tone scale is definitely one of the best for maintaining that tightness and focus as you scale your notes, however, with practice you can achieve the same results with longer five and even seven tone scales. Let’s take a look at the progression into more open type vowels and how best you can handle, or trick yourself into handling such vowels.

I love the open EEE vowel. When you’ve mastered the narrower vowels as above, it is quite easy to still maintain that focus with a more open vowel such as this without splatting—or losing focus. The key thing is to learn to discover your own anatomy a bit more. When in training, you should experiment by making slight adjustments. You’ll learn to fine tune that focus that keeps your voice spinning in top form and articulating each note to calculated precision. Running with an EEE whilst allowing the right amount of space in your mouth to do that can go a really long way towards sharpening your focus. The same applies with an open vowel like AAA.  Now here’s the thing. If this transition isn’t working, then the best way is to apply the narrower vowel up the scale, and then switch to a wider vowel on the way down. You’ll be amazed how easy and fluid this is, and how it helps you hold the note in on the wider vowels.

So, whatever you do, work your way into the broader vowels by first sharpening the projection of your narrower vowel. You’ll be glad you did as you begin to discover your voice and what you can do with it a bit more. I have created a special four-volume training module that is now available on Mkito.com. This brand new program will set the tone for focusing your notes as explained in this article.

SUBSCRIBE to My YouTube Channel TODAY... Click Here!

You are the instrument, learn to sing like a pro!


JOETT

Vocal Coach & Author "Letters from a Vocal Coach"
Private Singing Lessons
BUY Online Singing Lessons Course

Thursday, November 24, 2016

Jifunze Kuimba na Joett Mkito.com: Vocal Drills Volume 1

Kwa awamu nyingine tena, na tena safari hii kwa maboresho yalio fuata mahitaji muhimu katika kujifunza kuimba kupitia mtandao, ninawaletea toleo mpya kabisa Jifunze Kuimba na Joett Mkito Volume 1. Hili toleo ni muhimu katika kukuwezesha kuingia katika mstari wa mafunzo ambayo bila shaka, yatakuletea mafanikio ya haraka.

Kabla ya kuanza, hakikisha una download na kufanya zoezi langu la pumzi Mkito.com

Bila ya kuzungumza maneno mengi, nataka niwaachie toleo hili la kwanza (Vol. 1) msikilize mifano nakuendelea na mchanganyiko wa mazoezi ya sauti kwa takriban dakika 8. Mifano ipo. Nikusikiliza tu na kufuata hiyo mifano, na la msingi kabisa nikuachia sauti ifuate mkondo wake. Usilazimishe sauti. Iachie ifuate kinanda na maelekezo mwanana.

Muongozo wa Mazoezi

 • Download mazoezi Mkito.com
 • Weka kwenye CD au Flash Disk
 • Tumia chombo cha muziki cha kupigia CD/Flash au kama unatumia simu yako ya mkononi, hakikisha unaunganisha na speaker kupata sauti kubwa kulingana na sauti yako ukiimba. 
 • Fanya mazoezi ndani ya chumba na sio kwenye maeneo ya wazi, wala sio kwa kutumia simu yako ya mkononi na headset zake masikioni. 
 • Ku-Download PDF yenye maelekezo ya Volume 1, 2, 3 & 4 Bofya hapa!
 • Kusoma Press Release bofya hapa!

Ukiwa na maswali, jiskie huru kuniuliza, au soma nakala kadhaa nilizo andika:
Jifunze Kuimba: Umuhimu wa Kuelewa Madhumuni Ya Mazoezi
Jifunze Kuimba: Tatizo La Pumzi na Jinsi Ya Kulitatua
Jifunze Kuimba na Joett Mkito.com Vol. 1: Madhumuni ya Lip Rolls

Wewe ndie chombo halisi, jifunze kuimba kama pro!


JOETT
Vocal Coach
Madarasa ya Studio

Jifunze Kuimba na Joett Kupitia Mkito.com Yazinduliwa Rasmi

== PRESS RELEASE 24.11.2016 == Kwa mara ya kwanza kabisa, mtandao wa ku-download mziki wakitanzania Mkito.com, unajiunga na mwalimu mahiri wa sauti Tony Joett, kuwaletea watanzania huduma ya mafunzo ya sauti kwa wale ambao wangependa kujifunza kuimba kupitia mtandao na kwa gharama nafuu, nakupokea mafunzo yalio andaliwa kitaalamu kwa lugha ya Kiswahili na ambayo yataweletea mafanikio ya haraka na ya uhakika.

Joett ameandaa programu hizo za mafunzo ya sauti kwenye studio ya producer Lucci wa Transformax Records, ambae pamoja nae walikua majaji wa Airtel Trace Music Star Season 2 mwaka 2016. “Madhumuni ya kuandaa mazoezi haya maalum,” alisema Joett “nikuwawezesha watanzania kujifunza kuimba kwa urahisi, ili kutatua hili tatizo la vijana kuto jua pakugeukia kupata mafunzo haya ya kitaalamu na ambayo yanakuza vipaji kwa viwango vile vya kimataifa.”

Maandalizi ya programu hizi yamegawanywa katika volume ama toleo 4, ambazo toleo la kwanza ndio msingi; toleo la pili ni muendelezo; na toleo la 3 na la 4 zinaelekea kwenye viwango vya juu zaidi vya mafunzo ya kuimba, kwahivyo ili kupata mafanikio mwanafunzi atahitaji kuanzia tole la kwanza hadi kufikia la 4 na kwa mpangilio huo maalum, alafu hatimae kufanya mazoezi yote manne kwa pamoja. Kwa ujumula, mazoezi yote manne kwa pamoja yanachukua takriban dakika 30. Vile vile kuna zoezi stahiki la pumzi lililoandaliwa na Joett.

Watu wanaopenda kujifunza kuimba wataweza ku-download kila toleo kwa shilingi 250 tu, na kupata ushauri na muongozo kutoka kwa Joett kupitia Mkito.com na blog la JoettMusic.com.

Joett ambae pia hutoa mafunzo ya sauti ya ana kwa ana katika studio yake jijini Dar es salaam, ni mwalimu alie bobea kwa kipindi kirefu na anao uzoefu na utaalamu katika fani ya kufundisha sauti. Mafunzo anayotoa Joett yanasaidia kurekebisha matumizi ya sauti ili kuondoa tatizo sugu la kuimbia kooni; kupiga makelele wakati wakuimba; kuumia kooni na kukauka kwa sauti; na hujenga uwezo wa sauti ya mwimbaji kwenda juu na kwenda chini kwa urahisi na bila ya maumivu wala mateso ya aina yeyote.

Download Joett Vocal Drills Vol. 1 kuanzia alhasiri ya tarehe 24.11.2016 Mkito.com

Wewe ndie chombo halisi, jifunze kuimba kama pro!


JOETT
Vocal Coach
Madarasa ya Studio