Tuesday, September 27, 2016

Jifunze Kuimba: Tatizo La Pumzi na Jinsi Ya Kulitatua

Kama unatatizo la pumzi wakati unaimba—yaani unakwenda ukiishiwa mpaka koo linabana, basi unahitaji kujipanga na mazoezi ya pumzi ili uweze kukabiliana na hilo tatizo.

Ningependa kukanusha kitu kimoja. Mazoezi ya kukimbia, kubeba vyuma na kuogelea havitatui swala la uhaba wa pumzi katika kuimba. Havihusiani kabisa. Sasa nataka nikuonyeshe jinsi ya kutatua tatizo lako la kupumua ili uweze kuimba kwa urahisi.

Anza kupiga makofi kwa mwendo wa kawaida huku ukiingiza pumzi mdomoni hadi inajaza tumbo lako… kwa kufungua mdomo taratibu kama unapiga miayo (inakupa pumzi zaidi). Unavopiga makofi, kichwani uwe unahesabu. Pumzi ndani hadi unafika makofi manne, alafu hapo hapo toa pumzi kwa kupuliza hadi makofi manne; alafu rudia tena bila kusimama. Fanya hata mizunguko kumi na zaidi kabla ya kusimama. Tafadhali zingatia maelekezo hapo juu. Usikurupuke.

Shairi unaloimba hakikisha limeandikwa au limechapishwa na liko mbele yako. Kila sehemu za kuvuta pumizi, weka alama na kalamu nyekundu. Hiyo itasaidia kukujengea tabia ya kuimba na kupumua katika sehemu hizo ulizowekea alama… kwa wimbo huo.

Unaweza ku-download zoezi la pumzi hapa! Ingiza pumzi kwa ukimya, ili usisikie baridi inapita kooni. (Mfano wangu unasikika kwanguvu kwasababu ya kipaza sauti).

Natumaini umefaidika na maelezo hapo juu. Kama utakua na maswali yeyote, tafadhali andika hapo chini alafu nitakujibu ili na watu wengine pia waone suluhu la maswala ya pumzi.

JIUNGE na YouTube Channel Yangu Leo. Bofya hapa!

Wewe ndie chombo halisi, jifunze kuimba kama pro!


JOETT

Vocal Coach & Author "Letters from a Vocal Coach"




No comments:

Post a Comment