Mara kwa mara nakumbana na hili swala… kwamba watu wanaamini yakua kuna kitu kinachoitwa ‘kuimbia tumboni’. Kiukweli, hicho kitu hakipo kabisa. Nimeona niandike nakala hii ili kuweza kuwafahamisha vizuri.
Binadamu haongelei tumboni. Halikadhalika hawezi kamwe akaimbia tumboni.
Tunapozaliwa, kitu cha kwanza kabisa tunafanya ni kulia na kuvuta pumzi tumboni kama watoto wachanga ambao ndio kwanza tunaiona dunia. Hiyo ndio njia asilia ya sisi wanadamu kupumua. Nnanzia mbali ili mnielewe.
Kwahiyo basi, pumzi linapaswa kuvutwa hadi linaingia tumboni. Wanadamu tunapokua wakubwa, tunatabia ya kubadili jinsi ya kupumua kwa kupumulia ndani ya mapafu tu... na ndio chanzo cha matatizo. Ngoja nikupe mfano. Unapolala kitandani utakuta kwamba pumzi lako linaingia tumboni… utaona kabisa tumbo lina vimba na kushuka na lile pumzi. Sasa basi, twende kwenye kuimba.
Pumzi la kuimba ni lile letu asilia ambalo linaingia tumboni—ambapo kunayo nafasi kubwa zaidi hata ivyo—na ndicho kinachotuwezesha kuimba kwa urahisi bila ya kuishiwa na pumzi, na vile vile tukasikika vizuri. Maana bila pumzi, hakuna sauti. Kwa hivyo basi, binadamu hatuimbii tumboni bali tunavuta pumzi ndani ya tumbo (deep diaphragmatic breathing) ili kuimarisha sauti tunapoimba.
Natumaini mtakua mmenufaika na hii nakala yangu ya leo kuhusu swala nyeti la umuhimu wa tumbo lako katika kuhifadhi pumzi na kukuwezesha katika uimbaji.
Ku Download Zoezi La Pumzi Mkito, bofya hapa!
Muongozo wa Mazoezi
• Download Mazoezi Mkito.com
• Weka kwenye CD au Flash Disk
• Tumia chombo cha muziki cha kupigia CD/Flash au kama unatumia simu yako ya mkononi, hakikisha unaunganisha na speaker kupata sauti kubwa kulingana na sauti yako ukiimba.
• Fanya mazoezi ndani ya chumba na sio kwenye maeneo ya wazi, wala sio kwa kutumia simu yako ya mkononi na headset zake masikioni.
Na vile vile unaweza kupata maelekezo zaidi kwa kubofya nakala kadhaa nilizo andika hapa chini. Ukiwa na maswali, tafadhali jisikie huru kuniuliza. Ni muhimu sana kuelewa, na sio kufanya vitu kwa hisia bila muongozo panapo stahili. Tafuta ushauri!
Jifunze Kuimba: Umuhimu wa Kuelewa Madhumuni Ya Mazoezi
Jifunze Kuimba: Tatizo La Pumzi na Jinsi Ya Kulitatua
Jifunze Kuimba na Joett Mkito.com Vol. 1: Madhumuni ya Lip Rolls
Jifunze Kuimba na Joett Mkito.com: Vocal Drills Volume 2
Volume 1, 2 & 3 Jifunze Kuimba na Joett Mkito.com
Jifunze Kuimba na Joett Mkito.com: Vocal Drills Volume 4
Jifunze Kuimba na Joett Mkito.com Vol. 5
Wewe ndie chombo halisi, jifunze kuimba kama pro! Nawatakia mafanikio mema!
JOETT
Vocal Coach
YouTube Channel
Madarasa ya Studio
No comments:
Post a Comment