Basi nimekuandalia kila kitu. Cha kufanya ni kufuata maelekezo na kujumiaka na wenzio WhatsApp.
Nilikua nimesitisha huduma ya WhatsApp na kuhamia Crew na Telegram, lakini kwa mara nyingine tena nimeamua kurudi WhatsApp kwasababu watu wengi hupendelea zaidi app hiyo. Sasa basi, ukisha jiunga utapata muongozo wa jinsi zoezi hili linavo endeshwa, na pia utapata eBook (pdf) yangu yenye maelekezo kuhusu mazoezi ya sauti Joett Vocal Drills Vol. 1-7 ambayo yanapatikana Mkito.com.
Lakini ni muhimu kabla hujafanya lolote usome maelekezo hapa kwenye blog langu kwanza na ukiwa na maswali, ntayajibu kwenye group langu JOETT Voice Studio WhatsApp.
Kuna mazoezi ya ziada ambayo narushia WhatsApp na vile vile najibu maswali na kutoa ushauri kuhusu maswala ya uimbaji.
Maelekezo ya ziada kuhusu msaada huu maalum wa mafunzo utayapata hapa!
Kujifunza kuimba online inataka kujituma. Darasani pia inataka kujituma na kuhudhiria madarasa.
Ni muhimu ujijengee tabia ya kufanya mazoezi. Jitengenezee ratiba. Hata kama ni siku moja kwa wiki. Baada ya muda unazoe. Na inakua jambo rahisi kutekeleza bila ya kuona uzito.
Na la mwisho kabisa, kumbuka, mazoezi ya sauti hayana mwisho. Ni endelevu.
Nawatakia mafanikio mema!
JOETT