Wednesday, October 1, 2014

Joett Aachia Singo Mpya Akishirikisha Wasanii Chipukizi wa Bongo Flava G Fullah na Level One

PRESS RELEASE Octoba 1, 2014 -- Mwalimu wa kuimba na msanii wa ku-rekodi miondoko ya pop – Joett, anaachia singo yake mpya I’m Gonna Live Forever Octoba 13 2014, ambayo amewashirikisha wasanii wa bongo flava G Fullah na kundi la vijana wa kiume (boyband) lijulikanalo kama Level One. Vocals za trak hii zilirekodiwa na Max Rioba pale Authentic Records, Dar es salaam, na kuandaliwa na producer mahiri nchini Uingereza, Patrick Jonsson, ambae amefanya kazi na Joett kwa kipindi kirefu. Mixing pamoja na mastering ya trak hiyo imefanyika na sound engineer na producer King Penn (KP), wa Atlanta, Marekani,  ambae amefanya kazi na lebo ya Madonna ijulikanayo kama Maverick; Warner Bros, EMI, Beyonce, Solange, Columbia, 50 Cent, John Lennon Songwriters, MCA, The Big Boy Records, Def Jam, Dallas Austin, na mamia ya wasanii wa lebo ndogo zijuliakanazo kama Indie Labels. Joett, ambae hutoa singo moja tu kwa mawaka, aliamua kuwashirikisha vijana hawa ili kuwapa fursa ya kutoka katika viwango vya kimataifa, na amedhamiria kuendelea kufanya hivyo kwa miaka ijayo. “Ningependa sana kukuza vijana katika tasnia hii ya mziki, na hasa kuwashukuru mashabik pamoja na wadau wa mziki kwa ushirikiano wao enedelevu,” alisema Joett.

G Fullah alinyakuliwa na Joett toka kipindi cha ITV Hawavumi Lakini Wamo; Abdul Kagoi toka Epiq Bongo Star Search 2013; Rahym alitambulishwa kwa Joett na kaka yake, msanii wa bongo flava Mbongo Halisi, nakuchukuliwa na Joett kufundishwa kuimba. Nixon alidhaminiwa na mama yake kufundishwa sauti kwa Joett, alafu baadae Joett akamweka kwenye program yake ya misaada kwa wasanii chipukizi na hatimae kummpa mkataba wa ku-rekodi chini ya lebo yake – Joett Music. Kikundi cha Level One ni Abdul, Rahym na Nixon. Pakua trak hiyo kali kutoka tovuti la kibongo Mkito.com kuanzia Octoba 13, 2014.



Joett Music Publishing via ASCAP, USA.
Viber & WhatsApp on +255 787 364 045

No comments:

Post a Comment