Sunday, April 7, 2013

Letters from a Vocal Coach: Jinsi ya Kuzingatia Swala la Pumzi

Mafunzo ya kuimba ni kitu muhimu sana katika kujiendeleza kama muimbaji,  kwasababu huraisisha uimbaji wako kwa kuwezesha sauti yako kuendana na funguo za kinanda katika levo zote. Lakini pamoja na hayo, pumzi pia ni swala nyeti ambalo ningepende kugusia hapa.

Pumzi hadimu ni sauti hafifu, kwenye upande wa kuimba. Hili ni tatizo linalowakabili watu wengi. Jinsi ya kuepukana na upungufu wa pumzi ni kujizoesha kupumua kabla ya kila note. Yaani kabla ya kila kipande cha shairi. Hakuna wimbo ulioatungwa moja kwa moja bila hata sehemu ya kupumua...sidhani. Kwahiyo, kila pahala penye sehemu ya kupumua, tumia hiyo fursa kupumua. Kupumua kuimba ni tofauti na pumzi la kuzungumza.

Ili kua napumzi ya kutosha kuimba unahitaji kujaza pumzi kwa haraka zaidi. Jinsi yake ni kama nilivoelekeza kwenye zoezi la kupumua kwenye CD yangu Jifunze Kuimba na Joett. Tanua mdomo taratibu huku ukivuta pumzi kupitia mdomoni mwako tu...kama unavyopiga miayo, na kujaza pumzi hilo kwenye maeneo ya tumbo lako. Zingatia hilo, na ufanye hivyo (kwa haraka) kila kabla ya note.

Wewe ndio chombo halisi, jifunze kuimba kama pro!



JOETT
Vocal Coach & Author
Letters from a Vocal Coach

Download Joett tracks from iTunes, Amazon MP3, TuneCore.
Buy Joett CDs from A Novel Idea Bookstores Dar, Zanzibar, Arusha.
Nationwide CD distribution via Joett Music (Airtel Money, TIGO Money, M-Pesa).
Follow me on Twitter
Become a fan on Facebook 
Follow Joett On Facebook  

No comments:

Post a Comment